Kenya mtammiss sana Uhuru Kenyatta

Hata jana alijaribu kufanya ukora chief justice akampiga makumbo na kumkumbusha kuwa judiciary iko independent.
 
Ila anachota pesa WB na IMF anavyotaka!
 
Zile hazichotwi unavyotaka, lazima udhihirishe uwezo wa akili kubwa, huoni jinsi huwa mnahangaishwa hangaishwa kila mkiomba.
Uhuru akijisikia anaenda kuchota tu huoni kapewa hadi onyo
 
Uko sahihi kiongozi, anaweza kuja mwingine akajidai kuisigina katiba, lakini ni wazi kuwa atakuwa amejitoa akili na kuwa tayari kukutwa na yatakayomkuta. Katiba ikiweka bayana mipaka ya Rais na nini anaweza kufanyiwa anapokiuka katika huyo atakayeamua kuisigina anakuwa kajichagulia malipo yake (ama baada ya uongozi wake au ndani ya muda wa uongozi wake, kulingana na matakwa ya katiba). Kama katiba haimpi kinga ni lazima awe muoga hivyo huwezi ipuuza nguvu ya katiba. Katiba yetu ya TZ imemfanya Rais kuwa kiumbe asiyeguswa wakati wa utawala na hata akimaliza muda wake. Kenya haipo hivyo, ndiyo maana Kenyatta anaishia kuita majaji "wakora" tu ila hana cha kuwafanya. MK254 kasema Katiba Katiba Katiba, nami namuunga mkono kwa hili, wacheni Wakenya wafurahie matunda ya damu yao (haki haiji kirahisi)...sisi tuendelee kusubiri CCM wakijisikia!
 
Tatizo Jakaya alituachia mwisho tukasema anacheka cheka sana,ana safari sana nje,hadi watu wakatoa list of shame,jamaa akaona isiwe tabu akaamua kuwaachia mtu ambae hacheki cheki,sasa leo tumemkumbuka Jakaya,yupo zake Msoga katulia mzee wa watu hataki fujo na watanzania ambao bado hawajaelewa wanataka nini haswa.
Ila nadhani sasa tushaelewa tatizo letu kama watanzania lipo wapi.
 
Wewe leo umeongea kwa maarifa ila siku zingine huwa kichwa ngumu sana.
 
Lakini katiba mpya hamtapitisha kwa sababu nyie ni wapole sana na CCM haitaki katiba mpya kwa sababu itapunguza nguvu ya CCM
 
Huu Uhuru haujaanza na raisi wa awamu hii. Hata nyakati zake za utawala wake wa mwisho, mzee Moi alikuwa kishaa legeza. Unakumbuka vibaraka wake wakimshauri awachukulie hatua wasanii wa redykyulass. Alikataa na kusema ni bora wawache vijana wafurahishe watu!..
 
Redykyulass ndio waliipaisha comedy hadi ikawa kama tunavyoijua sasa hivi nchini Kenya. Enzi hizo comedy ilikuwa comedy kweli, jamaa walikuwa wajasiri sana kwa kumtania dikteta Moi bila uoga. Wapambe wake walikuwa wanamuambia kwamba hawa vijana wamekosa heshima, washughulikie. Ila waliponea kibahati bahati tu kwasababu 'mtukufu' alikuwa anaenjoy sana vibwanga vyao. Moi laughed his heart out at clips of Redykyulass- Standard Media Kuna clip yao ya enzi hizo ambayo niliiona hivi majuzi wakati wa mazishi ya 'MO1'. When Moi arrived in Heaven. [emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…