Kenya: Mtoto wa miaka 10 ajitahiri kwa kisu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368

Mvulana wa miaka 10 mkazi wa kijiji ya Itare nchini Kenya amejitahiri kwa kutumia kisu cha jikoni baada ya wazazi wake kushindwa kulipia gharama ya Ksh 1000/- ya kupewa huduma hiyo hospitali.

Mtoto huyo wa darasa la pili ameeleza chombo cha habari kimoja nchini humo kuwa alilazimika kufanya hivyo kwa kuhofia unyanyapaa atakaofanyiwa na wenzake ambao wao walifanyiwa toraha kipindi cha likizo ya mwezi Desemba.

Inaelezwa kuwa hali ya mtoto huyo kiafya sio nzuri tangu alipojifanyia kitendo hicho mwezi mmoja uliopita na awali alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kisii lakini wazazi wake walimrudisha nyumbani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Mwanaharakati wilayani Kisii, Samwel Momanyi ameomba serikali iingilie kati na kumsaidia mtoto huyo kupata matibabu kwani anapata maumivu makali sana hususani akijisaidia haja ndogo.

Mvulana huyo ameshindwa kuanza masomo shule zilivyofunguliwa leo, Jumatatu kutokana na afya yake kutoimarika.
 
Huo mtindo ulienea sana nyumbani mnamo mwaka 2011-2015. Nakumbuka mdogo wangu pia alijitahiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…