Kenya: Mwanafunzi achapwa viboko kwa kula chapati tano

Kenya: Mwanafunzi achapwa viboko kwa kula chapati tano

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
Mwanafunzi mmoja anapokea matibabu katika hospitali moja mjini Mombasa pwani ya Kenya baada ya kuchapwa viboko kwa kula chapati tano badala ya ile aliyopewa na shule.

Walimu wameshutumiwa kwa kumpiga mvulana huyo kwa kutumia bomba la kuchota maji lakini uongozi wa shule unasema ni wanafunzi wenzake waliofanyia hivyo.

Mvulana huyo wa miaka 13-ana alama nyeusi mwilini mwake, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani na kanda za video zilizosambazwa mitandaoni.

Wazazi wake wanasema shule haikuwafahamisha kuhusu tukio hilo hadi wiki iliyopita wakati mtoto wao alipozidiwa na ugonjwa.

Madaktari katika hospitali hiyo wanasema mvulana huyo aliumizwa figo vibaya na sehemu zake za siri pia zimejeruhiwa.

Maafisa elimu wa eneo hilo wameifunga shule hiyo kwa kutokidhi masharti ya usajili na usafi wa wizara hiyo baada ya kukaguliwa kufuatia tukio hilo.

Suala hilo limezua hasira miongoni mwa Wakenya mtandaoni:

“Hivi kweli ubinadamu ulienda wapi? Kwa nini mwalimu afanye hivi, kwa sababu ya chapati tu? Kufundisha sio kazi, ni shauku, jukumu alilopewa na Mungu. Sio mteso kwa wadogo zetu. Hili limevunja moyo wangu,” @IamAlanjenga alitweet.

“Jiulize kama huyu ni mtoto wako utamchukuliaje? Natumai watamfungulia mashtaka ya kujaribu kuua!” @NjeriMuchina2 alisema.

bf9743d3-b832-450c-b556-ad62ce3961c1.jpg
 
Kuna wakenya wanaonunua nyanya maeneo ya Tarakea na Iringa huwa wanashangaa kuona jinsi ambavyo kwa buku unapata chapati za kutosha na mchuzi juu. Sasa nimewaelewa.
 
Kuna wakenya wanaonunua nyanya maeneo ya Tarakea na Iringa huwa wanashangaa kuona jinsi ambavyo kwa buku unapata chapati za kutosha na mchuzi juu. Sasa nimewaelewa.
maisha ya kwao tofaut na Tz
 
Nimegundua fursa ya biashara; nitaanza kusafirisha chapati kwenda kenya ili nikauze huko.

Watz hiyo ni fursa, you have to say sorry for the kid but at the same time take it as an opportunity for doing business.

MK254 🤣
 
Back
Top Bottom