Kenya: Mwenye nyumba amuua mpangaji kwa kumdai takriban Tsh 57,000

Kenya: Mwenye nyumba amuua mpangaji kwa kumdai takriban Tsh 57,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwenye nyumba Ngángá Gitau, amemchoma visu mpangaji wake hadi kufa Warren Jirongo (26) baada ya kushindwa kulipa kodi ya mwezi Januari

Wakazi wa eneo hilo wamemzonga mwenye nyumba huyo kwa hasira na kuchoma nyumba zake moto baada ya yeye kumuua kijana huyo

Kijana huyo ni yatima ambaye alikuwa anafanya kazi ya kukusanya uchafu majumbani. Majirani zake wamemsifu kama kijana anayejituma kwenye kujitafutia riziki

Wakazi hao waliingia mitaani na silaha kumtafuta mwenye nyumba huyo ambaye alikuwa amejificha, Polisi walifika eneo la tukio na kuwasambaratishwa raia hao japo uharibifu ulikuwa tayari umeshafanyika.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha mji huku uchunguzi juu ya kifo chake ukiendelea

CHANZO: TUKO
 
Hawa jamaa wenyewe si matajiri wanasemaga??? Sa unamuuaje Mwana kwa kahela ka bia tano ??? Kenya kuna shida jamani muwe mnaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini huyo marehemu kawa mgumu kulipa pesa ya watu mpaka ameuwawa na jinsi mapolisi ya Kenya yanavyopenda milungula wala hatakaa sana gerezani ila marehemu nina uhakika atazikwa na ataoza
 
Back
Top Bottom