Kenya na India Zaipiku Tanzania Kwa Mauzo ya Tanzanite

jnuswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,270
Reaction score
549
Hii habari ni mbaya sana kwetu Watanzania, lakini pia ni fundisho kwetu tujisahihishe kujua ni wapi tunapokosea katika mikakati ya kukuza uchumi wetu. India imeweza kuuza Tanzanite yenye thamani ya Dola million 300 Kenya million 100 na Tanzania million 38.

Inakuwaje madini ambayo yanapatikana Tanzania pekee duniani hizo nchi zinatupiku ? Inaumiza sana kusikia mambo kama haya.

attachment.php

Nchi za Kenya na India zimeipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee.

Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa jana kwamba kwa mwaka jana, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Kamishna Masanja alisema mwaka jana pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.

"Katika kipindi hicho cha mwaka jana, India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India," alisema Masanja.

Bila kumtaja jina, Kamishna huyo alisema mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka nchini Marekani aliwahi kumuuliza iwapo kuna migodi ya tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.

Alisema zaidi ya asilimia 80 ya tanzanite inayopatikana Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, Manyara huuzwa kwa njia za panya nje ya nchi na kwamba Serikali imeanza kuchukua hatua.

"Serikali inakusudia kuunda kikosi kazi kitakachojumuisha askari kutoka vyombo vyote vya ulinzi na usalama kukabiliana na utoroshaji madini nje ya nchi."

Alisema hivi karibuni, wizara itawasilisha muswada bungeni kurekebisha Sheria ya Madini Namba 6 ili kumpa mamlaka Kamishna wa Madini kutaifisha madini yote yanayokamatwa yakisafirishwa kinyume cha sheria.

"Tunataka sheria ya madini ifanane na ile ya misitu inayotaifisha mazao yote ya misitu yanayovunwa kinyume cha sheria, tofauti na sasa ambapo tunalazimika kusubiri uamuzi wa Mahakama kutaifisha madini iwapo watuhumiwa wanatiwa hatiani," alisema.

Hadi sasa, Serikali imekamata na kutaifisha madini yenye thamani ya zaidi ya Sh15 bilioni yaliyokamatwa yakitoroshwa nje ya nchi baada ya watuhumiwa kutiwa hatiani na Mahakama.

"Tuna mpango wa kujenga kituo maalumu cha madini kitakachojulikana kama Madini House kitakachokuwa na ofisi zote za kununua na kuuza madini ya vito ili kudhibiti biashara holela," alisema Masanja.

Alisema katika kituo hicho kutakuwa na huduma za kodi na malipo mbalimbali ya Serikali pamoja na usafiri wa helikopta za kusafisha madini kwenda viwanja vya ndege ili kuepuka wizi na uvamizi njiani.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ngosi Mwihava aliwataka Watanzania kushiriki katika vita dhidi ya uhujumu uchumi na kwamba juhudi za Serikali za kupambana na wanaotorosha madini nje ya nchi haziwezi kufanikiwa bila ushiriki wa umma kwa kutoa taarifa kwa vyombo na mamlaka husika.

Chanzo:Mwananchi
 
hua mabroker wanapeleka nairobi kuuza kwa bei nzuri na wakenya wanapeleka india
 
Hii habari ni mbaya sana kwetu Watanzania, lakini pia ni fundisho kwetu tujisahihishe kujua ni wapi tunapokosea katika mikakati ya kukuza uchumi wetu. India imeweza kuuza Tanzanite yenye thamani ya Dola million 300 Kenya million 100 na Tanzania million 38.

Inakuwaje madini ambayo yanapatikana Tanzania pekee duniani hizo nchi zinatupiku ? Inaumiza sana kusikia mambo kama haya.

nimeona hii taarifa roho ikaniuma sana inasemekana kenya kuna stock kubwa sana ya tanzanite na ndio moja ya thamani inayoipandisha kiuchumi kila kukicha kenya
 
Hivi Serikali ipo wapi? ndiyo maana Kagame anamdharau jamaa? ushauri aliyowahi kuutoa mama kilango hadi leo haujawahi kutekelezwa, sijui jamani,
 
Ccm oyeeeh!Waache waongoze tu kama le profeseli hajui kwa nini nchi yake ni masikini ulitegemea nini???Mbona hata mlima kilimanjaro wazungu wana jua upo kenya!
 
unnamed%2B(17).jpg
unnamed%2B(19).jpg
hawa ndio wafanya biashara wakubwa wa tanzanite mleta mada ni mkweli
 
Hivi Serikali ipo wapi? ndiyo maana Kagame anamdharau jamaa? ushauri aliyowahi kuutoa mama kilango hadi leo haujawahi kutekelezwa, sijui jamani,

Usianze kulaumu bila ktafakari.tatizo la tanzania kuwa na wanasiasa wababaishaji.nasema hili watoroshaji wakubwa wa madini yetu sio tanzanite pekee hata dhahabu ruby nk ni wachimbaji wadogowadogo ambao kwa bahati mbaya wanatetewa sana na wanasiasa.ili hali inajulikana udhibiti wao ni mgumu sana.katika kujua mapatao yao na control ya mauzo ikiwa pamoja na ulipaji kodi.
 
Asilimia 80 ya madini aina ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania, yanatoroshwa nje ya nchi na wafanyabiashara wasio waaminifu, huku nchi ikiambulia asilimia 20 tu ya madini hayo yanayozalishwa eneo la Mererani mkoani Manyara.

Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Masanja, amesema hayo wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Vito, yanayofanyika jijini Arusha na kukutanisha washiriki zaidi ya 500, huku kampuni 69 zikishiriki maonyesho hayo.

Masanja ametoa mfano wa mwaka 2013 ambapo Tanzania ilipata mapato yanayofikia dola za Marekani milioni 38 kutokana na Tanzanite, wakati Kenya walipokea Tanzanite yenye thamani ya dola milioni 100, huku India ikipata dola milioni 300 za madini hayo.

Amesema kuwa kutokana na hali hiyo, serikali imeamua kujenga jengo la kuuzia madini hayo na litakapokamilika hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza madini hayo nje ya jengo hilo kama ilivyo sasa.
 
Dah kiukweli wafanya haraka na wadhibiti
 
Naona kitu muhimu kwa Tanzania ni kuweka sheria zitakazotumika...commissions zitakazo chunguza na kutoa mwelekeo mzuri wa kufwatwa..kenya iko na commission ya minerals iliyotoa jinsi ya kupata mapato kutokana na madini na jinsi ya kugawana baina ya serikali, makampuni na wananchi
 
Hii ndo Tanzania katika muendelezo wake wa maajabu yake duniani Kenya, India zaipiku Tanzania mauzo ya tanzanite.

Arusha. Nchi za Kenya na India zimeipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee.

Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa jana kwamba kwa mwaka jana, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Kamishna Masanja alisema mwaka jana pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.

"Katika kipindi hicho cha mwaka jana, India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India," alisema Masanja.

Bila kumtaja jina, Kamishna huyo alisema mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka nchini Marekani aliwahi kumuuliza iwapo kuna migodi ya tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.

Alisema zaidi ya asilimia 80 ya tanzanite inayopatikana Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, Manyara huuzwa kwa njia za panya nje ya nchi na kwamba Serikali imeanza kuchukua hatua.

"Serikali inakusudia kuunda kikosi kazi kitakachojumuisha askari kutoka vyombo vyote vya ulinzi na usalama kukabiliana na utoroshaji madini nje ya nchi."

Alisema hivi karibuni, wizara itawasilisha muswada bungeni kurekebisha Sheria ya Madini Namba 6 ili kumpa mamlaka Kamishna wa Madini kutaifisha madini yote yanayokamatwa yakisafirishwa kinyume cha sheria.

"Tunataka sheria ya madini ifanane na ile ya misitu inayotaifisha mazao yote ya misitu yanayovunwa kinyume cha sheria, tofauti na sasa ambapo tunalazimika kusubiri uamuzi wa Mahakama kutaifisha madini iwapo watuhumiwa wanatiwa hatiani," alisema.

Hadi sasa, Serikali imekamata na kutaifisha madini yenye thamani ya zaidi ya Sh15 bilioni yaliyokamatwa yakitoroshwa nje ya nchi baada ya watuhumiwa kutiwa hatiani na Mahakama.

"Tuna mpango wa kujenga kituo maalumu cha madini kitakachojulikana kama Madini House kitakachokuwa na ofisi zote za kununua na kuuza madini ya vito ili kudhibiti biashara holela," alisema Masanja.

Alisema katika kituo hicho kutakuwa na huduma za kodi na malipo mbalimbali ya Serikali pamoja na usafiri wa helikopta za kusafisha madini kwenda viwanja vya ndege ili kuepuka wizi na uvamizi njiani

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ngosi Mwihava aliwataka Watanzania kushiriki katika vita dhidi ya uhujumu uchumi na kwamba juhudi za Serikali za kupambana na wanaotorosha madini nje ya nchi haziwezi kufanikiwa bila ushiriki wa umma kwa kutoa taarifa kwa vyombo na mamlaka husika.

Chanzo:Mwananchi
 
Hii habari ni mbaya sana kwetu Watanzania, lakini pia ni fundisho kwetu tujisahihishe kujua ni wapi tunapokosea katika mikakati ya kukuza uchumi wetu. India imeweza kuuza Tanzanite yenye thamani ya Dola million 300 Kenya million 100 na Tanzania million 38.

Inakuwaje madini ambayo yanapatikana Tanzania pekee duniani hizo nchi zinatupiku ? Inaumiza sana kusikia mambo kama haya.

Hiyo biashara haifanywi na serikali inafanywa na watu binafsi.Bei nzuri ziko kenya na India.Wanunuzi wa Tanzania na nyie si mtoe bei nzuri kwa wachimbaji wadogo kama wenzenu wakenya na wahindi wa india?
Wakenya na wahindi wananunua kwa bei kubwa kuliko watanzania na kuuza india na marekani.

Namsifu Muhongo aliposema watanzania wana mitaji ya kuuza juice na maji tu gesi na madini hawawezi.Hivi wafanyabiashara watanzania hawajui soko bora liko marekani na india? Nunueni kwa bei kubwa watanzania watawauzia halafu kauzeni huko ulaya na marekani na india mtajirike
Kila kitu mnalaumu siasa na Chama hivi hao wakenya hizo Tanzanite huwa wananunuliwa na chama cha KANU,CORD AU ODM?
 
Kama ningekua mmoja Wa viongozi swala la madini ya Tanzanite lingenifanya nione aibu ninapokutana na viongozi Wa nchi jirani. Mambo haya japo viongozi ni Wa kuyafuatilia na kuhakikisha faida kwa nchi ,inafedhehesha kila mtanzania ukiyasikia. Wakenya wazalendo sana kwa nchi yao ,yaani ata tanzanite za kuiba zinaipatia Kenya dola milioni 100 ,na India dola milioni 300,wakati Tanzania dola milioni 38; na tanzanite ndio yenye thamani kuliko dhahabu na almasi,na kupatikana Tanzania tu,dah! Tanzanite yenye uzito wa chini ya kilo ina thamani ya dola milioni moja. Ukweli viongozi wajivishe uzalendo,aibu ikifichwa ndani itaanza kuja tokea nje. Tumekataa kuhusika meno ya Tembo kwa ndege ya raisi Wa China,bado linatupiwa hili la kuachilia tanzanite,yaani watu wanakula huku wanatucheka ,lol ,kweli mungu atusaidie.
Serikali kudhibiti utoroshwaji wa madini nje ya nchi

http://issamichuzi.blogspot.com/2014/11/serikali-kudhibiti-utoroshwaji-wa.html
 
Usianze kulaumu bila ktafakari.tatizo la tanzania kuwa na wanasiasa wababaishaji.nasema hili watoroshaji wakubwa wa madini yetu sio tanzanite pekee hata dhahabu ruby nk ni wachimbaji wadogowadogo ambao kwa bahati mbaya wanatetewa sana na wanasiasa.ili hali inajulikana udhibiti wao ni mgumu sana.katika kujua mapatao yao na control ya mauzo ikiwa pamoja na ulipaji kodi.

Hata kama ni wachimbaji wadogo, mbona hao wakubwa wanasomba udongo ,wanasamehewa kodi, na wanachangia 3% , bado si jawabu
 
Back
Top Bottom