Kenya na India Zaipiku Tanzania Kwa Mauzo ya Tanzanite




Nchi za Kenya na India zimeipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee.

Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa jana kwamba kwa mwaka jana, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Kamishna Masanja alisema mwaka jana pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.

"Katika kipindi hicho cha mwaka jana, India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India," alisema Masanja.

Bila kumtaja jina, Kamishna huyo alisema mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka nchini Marekani aliwahi kumuuliza iwapo kuna migodi ya tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.

Alisema zaidi ya asilimia 80 ya tanzanite inayopatikana Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, Manyara huuzwa kwa njia za panya nje ya nchi na kwamba Serikali imeanza kuchukua hatua.

"Serikali inakusudia kuunda kikosi kazi kitakachojumuisha askari kutoka vyombo vyote vya ulinzi na usalama kukabiliana na utoroshaji madini nje ya nchi."

Alisema hivi karibuni, wizara itawasilisha muswada bungeni kurekebisha Sheria ya Madini Namba 6 ili kumpa mamlaka Kamishna wa Madini kutaifisha madini yote yanayokamatwa yakisafirishwa kinyume cha sheria.

"Tunataka sheria ya madini ifanane na ile ya misitu inayotaifisha mazao yote ya misitu yanayovunwa kinyume cha sheria, tofauti na sasa ambapo tunalazimika kusubiri uamuzi wa Mahakama kutaifisha madini iwapo watuhumiwa wanatiwa hatiani," alisema.

Hadi sasa, Serikali imekamata na kutaifisha madini yenye thamani ya zaidi ya Sh15 bilioni yaliyokamatwa yakitoroshwa nje ya nchi baada ya watuhumiwa kutiwa hatiani na Mahakama.

"Tuna mpango wa kujenga kituo maalumu cha madini kitakachojulikana kama Madini House kitakachokuwa na ofisi zote za kununua na kuuza madini ya vito ili kudhibiti biashara holela," alisema Masanja.

Alisema katika kituo hicho kutakuwa na huduma za kodi na malipo mbalimbali ya Serikali pamoja na usafiri wa helikopta za kusafisha madini kwenda viwanja vya ndege ili kuepuka wizi na uvamizi njiani.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ngosi Mwihava aliwataka Watanzania kushiriki katika vita dhidi ya uhujumu uchumi na kwamba juhudi za Serikali za kupambana na wanaotorosha madini nje ya nchi haziwezi kufanikiwa bila ushiriki wa umma kwa kutoa taarifa kwa vyombo na mamlaka husika.

Chanzo:Mwananchi

http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...97296/2527420/-/item/0/-/b57biiz/-/index.html
 
Nchi hii haina viongozi wala uongozi kwani kila mtu anajifanyia anavyojua.
Mkapa ndiye alianza kuharibu baada ya kumtoa Ally Mchumo kutoka ubalozini South Africa baada ya kuorganise kampuni 2anzanite one na kumpeleka Mererani kupewa maeneo makubwa huku wananchi wakitengwa.
Hawa makaburu walii-leble tanzanite kuwa inatoka afrika kusini.
Walishauriwa sana hawa mawaziri kujenga na kuendesha minada ya tanzanite Arusha pamoja na kui-prossess hapo badala ya kuiuza ghafi wakapuuzia. Si bure huenda nao ni madalali wa wahindi ndo maana wanatudharau. Aibu kubwa sana hii kwa wote wanaohusika kutuhujumu.
Tubadilikeni basi kwa kuwapigia kura ya hapana kuanzia kwenye katiba ili tujikomboe.
 
Tanzania ina urasimu sana kwenye mambo ya kibiashara wakati saivi soko lote la East Afrika liko Nairobi, ukitaka kununua au kuuza chochote nenda Nairobi
 
Moderator peleka hii habari jukwaa la wakenya

Ndugu acha watu wajadili na kujiuliza juu ya hiki kinachotokea na inatakiwa tujue TANZANITE ONE inavyosemekana inamilikiwa na mtoto wa JK tena yule mbunge sasa inamaanisha huwa anapitia njia za panya kuuza hiyo TANZANITE?
 
Tanzanite imeanza kuchibwa miaka ya 80s au 90s, muda wote huo hawajaweza kuyadhibiti yasitoloshwe kinyemela? Leo hii wanakuja na blaa blaaa, (mpango mkakati, kikosi kazi, mkakati maarumu). Na kipindi cha nyuma tanzanite ilikuwa inapatikana tu juu juu, hata kwa jembe la mkono unachimba na unapata, leo hii tanzanite ipo umbali unakaribia kilometa 1 kwenda chini. Kama sikosei mwaka majuzi Kenya ilizawadiwa ndege, kwa kushika namba 1 kwa uuzaji, wakifuatiwa na south africa.
 
Hili jambo si jipya. Limefhamika kwa miaka mingi tu. Tunapopiga kelele kwamba nchi hii inakosa leadership watu wengine wanabisha. Hii ni indicator ya uongozi dhaifu...... na lugha ya " Tuna mpango wa kujenga kituo maalumu cha madini kitakachojulikana kama Madini House kitakachokuwa na ofisi zote za kununua na kuuza madini ya vito ili kudhibiti biashara holela" inatia kichefuchefu. This should have been done years back!
 
Dr.Slaa aliwataja mafisadi papa pale mwembe yanga hamkuwaelewa?wa kwanza alikuwa..... ndio wanaoimaliza nchi!mlitegemea nn?
 
RUCCI

Inauma sana na inatia aibu.Iweje madini yapatikane Tz wenzetu waongoze kwa mauzo.We,Tanzania we are too humble na atuthamini vile Mungu alivyotupa.Wangetupa na mauzo ya Karafu uenda na hilo wangeongoza Wakenya japo karafuu inapatikana Zanzibar.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna mchimbaji mdogo wala mkubwa anayefanya kwa uwazi hii biashara ya tanzanite, kila mmoja ana njia zake za panya anazozijua yeye. Njia zao kuu za kuvusha huo mzigo ni airport ya kia na boda la Namanga, mchana kweupee.
 
Watu wengi hamuelewi hii biashara inavyofanyika mimi binafsi nafanya hii biashara kusema mawe yanapitishwa kwa magendo si kweli sbb serikali wala haikatazi kusafiri haya mawe yakiwa yamefanyiwa carting mi husafirisha tena sio peke yangu na watanzania we zangu kibao unalipia tu wizarani na hamna hata rushwa yoyote .wahindi ndio ni wanunuzi wa kubwa sana mtu anakuja kununua mawe ya 1ml dolla wewe utakataa kumuuzia maana wanauziwa na watanzania tu wanaochimba.na kunakitu watu hawajui kuhusu wahindi niwatu wanaojua kucontro soko yani na maanisha kwa mlaji wa mwisho huko wamebana price kiasi kwamba unaamua tu kumuuzia yeye ukiangalia bei ya rejareja nje tofauti sio kubwa sana na hapa yeye anamjua mpaka broker wakumpelekea Beyoncé we utamjulia wapi? Ndio maana wao wanaonekana wanauza zaidi kuliko hapa kinachozungumzwa ni soko la nje maana mawe yote ya nanunuliwa hapa.ngoja nitolee mfano Mozambique wana contro ruby pale ni watanzania na wachimbaji wengine pia walitoka tanzania tena watu wa kawaida tunawauzia wa Thailand huyo Mozambique hata m Thai hamjua
 

umeelezea vizuri sana.
 
Tupe ushahidi / link / or something lika that....!
This is not proved.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…