G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Hizi nchi kwa huu utawala hazitakuwa na mwisho mzuri. Ukiona hadi Raila analalamika basi shida ni lazima ipo kwa Rais wetu. Tumwambie ukweli.
Kwa takwimu hizi za madereva 51 kati 53 waliokutwa na Corona kwenye mpaka kati ya Kenya na Tanzania kuwa watanzania basi ni lazima jambo lifanyike. Na pia haiwezekani mipaka yote tuwe ni sisi tu! Lazima sisi ndiyo chanzo cha matatizo! Tukiendelea hivi tuna mwisho mbaya. Tusiendelee kamwe kujidanganya aslani.
Ma RC wanafunga mipaka bila kutoa muda, kila RC anajitamkia lake. Wakati Shigela akisema anafunga mpaka kwa kuwa Kenya wanaleta Corona Tanzania, yeye mama Anna Munghwira kule Kilimanjaro anasema ni kutokana na Kenya kutokuwa fair kibiashara kwa Tanzania. Tuchukue kipi?
Tuache siasa mfu. Wakuambiwa ukweli aelezwe ukweli. Haiwezekani nchi zote za mpakani zione tatizo kwa Tanzania. Tuache kujikomba kwa Rais tumueleze ukweli kuwa aina yake ya siasa ni ya hatari kwa ustawi wa nchi.
Na tangia lina ma RC wakatangaza kufunga mipaka?
Eti Corona imeisha Tanzania. Ni upuuzi kuamini hivyo!