Ni kama wametuvua nguo
Mambo waliyoyafanya ukiwa unamtolea mfano mtu wa kunyooka kwao kidemokrasia atakaepinga basi huyo ameshindikana. Na mfano sio wa mbali eti South Africa au Botswana
Heshima za viongozi wetu ambao walikuwa vinara wa Siasa za Waafrika ziko wapi
Hawakutuachia katiba nzuri na walikijua udhaifu wa katiba yetu.
Walituhinikiza tuingie kwenye mfumo wa Vyama vingi kabla ya kubadilisha katiba, walitutia mtegoni => tukafunga ndoa kwanza, uchumba tutafanya tukishaowana
Wakaanzisha CCM B za kumwaga, mpaka leo ni vigumu kutenganisha pumba na mchele
Lakini yote hayo kwa faida ya nani ?