Kenya ni nchi inayoongoza kwa rushwa tena inawezekana ikawa kwa Afrika namba moja

Kenya ni nchi inayoongoza kwa rushwa tena inawezekana ikawa kwa Afrika namba moja

Mbolabilika

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2019
Posts
2,128
Reaction score
2,867
Watanzania waanika Kenya kwa kuwaitisha hongo kubatilisha matokeo ya COVID-19

- Madereva hao huitishwa hongo ya KSh2,000 katika mpaka wa Namanga ili matokeo yao ya COVID-19 yaweze kusoma hawana virusi

- Malalamishi hayo yaliwasilishwa mbele ya Naibu Waziri wa Afya nchini humo

- Katibu katika Wizara ya Afya Rashid Aman alitangaza kuwa visa 105 zaidi vya maambukizi ya COVID-19

Madereva wa malori kutoka nchini Tanzania, ambao hutumia mpaka wa Namanga kwa safari zao, wamezua malalamishi kuwa huwa wanaitishwa hongo ya KSh2000 ili matokeo yao ya COVID-19 yabatlishwe.

Malalamishi hayo yaliwasilishwa mbele ya Naibu Waziri waAfya nchini humo, Godwin Mollel, siku ya Jumatano, Juni 10.
Tanzania View pictures in App save up to 80% data.
Picha ya mpaka wa Namanga ambayo madereva hao Watanzania hutumia katika safari zao. Picha: Nation.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, Mollel alifanya mkutano na madereva hao ili kusikiliza changamoto zinazowakumba katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona.

"Sisi kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tunaambiwa tuna Corona, na mimi wiki mbili nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina Corona na sijawahi kutumia dawa yoyote mpaka sasa hivi, na tukipimwa tunaombwa 2000 ya Kenya ili watupe majibu kwamba hatuna Corona" alisimulia dreva moja kwa jina Japhet Jeremiah.
Tanzania View pictures in App save up to 80% data.

Picha ya Afisa wa polisi akipokea mlungula kutoka kwa dereva. Madereva hao huitishwa hongo ya KSh2,000 katika mpaka wa Namanga.Picha: UGC.

Katika kauli yake, Mollel alisema kuwa serikali ya Tanzania inafahamuchanhamoto ulioko kwenye mpaka huo na itaongeza kasi katika kuhakikisha suluhu inapatokana.

"Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa" alisema Mollel.

Mollel aliongezea kwamba changamoto hiyo katika mpaka wa Namanga ni suala mtambuka, ambalo linahusisha Wizara zaidi na ambalo ni la kibiashara na uchumi kati ya mataifa mawili.

Mnamo Jumatano, Jun 10, katibu katika Wizara ya Afya Rashid Aman alitangaza kuwa visa 105 zaidi vya maambukizi ya COVID-19 vimeripotiwa nchini na kufanya idadi ya wagonjwa kufikia 3,094.

96 kati yao ni Wakebya na wengine tisa kutoka mataifa ya kigeni.

Kati ya 105 hao waliopona 43 wanatoka Nairobi, Busia 18, Mombasa 11, Turkana 7, Migori 6, Kwale 5, Kiambu 5, Kilifi 3, Machakos 3, Taita Taveta 3 , Kisumu 2, Uasin Gishu 1, Kajiado 1, Garissa 1, . Siaya 1.

Visa vyote vya Busia, Turkana, Uasin Gishu, Kisumu na Taita Taveta ni madereva wa malori kutoka Malaba, Nadapal, Turbo, Kisumu ya Kati na Taveta.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp.

Source: Watanzania waanika Kenya kwa kuwaitisha hongo kubatilisha matokeo ya COVID-19
 
Michinga Midanganyika wenye hawajielewi. Mmemaliza kuuwa Mbowe
 
Screenshot_2020-06-13-20-19-43-617_com.facebook.katana.jpg
 
Back
Top Bottom