Kenya ni taifa la wakoloni, hawajawahi kuondoka

Kenya ni taifa la wakoloni, hawajawahi kuondoka

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kenya ni taifa ambalo halijawahi kuupata Uhuru wake hata kidogo. Hata Mzee Jaramongi Odinga alipoandika kitabu chake cha "Not yet Uhuru" alimaanisha lakini walimpiuza.

Wakenya ni wakimbizi kwenye taifa Leo, wanazalisha kwa manufaa ya wakoloni. Wakenya ni manamba kwenye nchi za wakoloni na wanalipa Kodi huko na kuzeekea huko.

Wakenya. Waliobaki Kenya wengi wao hawana cha kupoteza; hawana ardhi, nyumba Wala mifugo (properties), hivyo hawaogopi kupoteza chochote.

Wakoloni wamekota mizizi yao Kenya kisiasa, kiuchumi na kijeshi kuhakikisha kuwa maslahi yao Yako salama milele.

Kenya ni miongoni mwa mataifa ya Afrika yanayoihujumu OAU (AU) kwenye mpango yake ya kujiimarisha kama bara linalojitegemea.

Migomo Kenya ni harakati za ukombizi kutoka kwa wakoloni.
 
Nchi ya migomo hata kama wametunga katiba nzuri. Katiba nzuri peke yake haitoshi kuketa ahueni kwa wananchi bali uchumi mzuri na utashi
 
Kwani huko kwenu kukoje?
Huku kwetu Kuna maskini jeuri. Kuna kabila Moja TU linalotangatanga huku na huko duniani likitafuta fedha kwa gharama yoyote. The rest aaaah, maisha yanakwenda TU kwenye miji yao. Kuna options nyingi kwenye Kila eneo la maisha. Kila kaya inayo mali wasiyotaka iwaponyoke,
 
Tanzania ni Nchi nzuri Sana kwa raia Mmoja mmoja, issue labda ni hao CCM tu.
CCM sio tatizo hapa hata kidogo, kwa kuwa hatuna chama kingine madhubuti so far cha kuikabidhi nchi kwao. CCM ni kama jino laini kwasasa linalokosa mtu wa kuling'oa kwasababu ya hofu ya maumivu, kuwa na pengo au kupoteza uzuri wa kinywa. kule Kenya KANU iliondoshwa na vikundi vya wahuni TU visivyokuwa na dira, lakini hakuna chama imara chenye sera mbadala na KANU. Ndio maana Kenya ina oscillate palepale kama pendulum bob. Pamoja kuwa na katiba nzuri na mahakama nzuri.
 
Ivi odinga alishinda kile cheo cha ukubwa wa Africa?
 
Hafai kupewa cheo kile. Kenya inaamini kwenye utegemezi wa wazungu kwenye kila jambo. Atailemaza Africa kwa msaada kutoka kwa watesi wetu.
 
Pamoja na matatizo ya Kenya hata sisi hatuko huru, tanzanite yetu Ila Kenya wanauza kutuzidi.
Huelewi? Kenya mkoloni hajawahi kuondoka tangu enzi hizooo!!;Bado wameing'ang'ania ardhi ya wakenya, mbuga na rasilimali nyingine. Wakati Tanzania na Uganda wanahangaika na kuwanyang'anya wakoloni na wahindi mali zao kule Kenya hawakufanya hivyo, walibaki na makazi Kibira TU na maeneo yasiyokuwa na rutba. Ndio maana njaa haiondoki Kenya kwakuwa ardhi yao safi ya kilimo wahuni wanalima maua, chai, pareto na kahawa kupeleka kwao Ulaya.

Sio ajabu kuona tanzanite ikiuzwa sana Kenya kwakuwa Kuna watu wenye mitaji mikubwa ya kukunua tanzanite.
 
Pamoja na matatizo ya Kenya hata sisi hatuko huru, tanzanite yetu Ila Kenya wanauza kutuzidi.
Hii ni tofauti kabisa kaka. Kuna wanasiasa hapa wanalilia tuwe na katiba mpya na demokrasia kama ya Kenya. Kaka Kenya wanavyo hivyo vyote lakini bado kuna watu wanatekwa, wanalala na njaa, hawana ajira, wanagoma kila siku, wanaikimbia nchi yao kila siku. Afrika shida yetu sio Katiba nzuri, sheria wala demokrasia. Nchi za waarabu hakuna kabiba nzuri, demokrasia nzuri wala sheria kama za ulaya na marekani lakini mambo yao ni mazuri, kila mtu anapenda aende Dubai, Qatar, Oman, Saudi, Misri akale bata. Watu kama Lissu ni waongo waongo waongo kabisa, hata wakipewa nchi na kubadilisha katiba hali ya wananchi na nchi vitabaki vilevile au kurudi nyuma kabisa. Shida yetu ya msingi ni:
1. Nchi za magharibi kutuchagulia viongozi wetu kwaajili ya maslahi yao hata kama viongozi hao hawapendwi au ni madikteta- Masilahi.
2. NATO, EU, WB, WTO, IMF, ICC, na UN kuhodhiwa na nchi za magharibi- Unfairness.
3. Wizi wa viongozi wetu wenyewe - ubadhilifu/rushwa
4. Ukosefu wa mitaji
5. Ukosefu wa technolojia
6. Ukosefu wa wataalamu kwenye ngazi zote kuanzia kwenye uongozi mpaka kwenye utendaji na uzalishaji.

Mambo haya ndiyo yanasababisha hata aende nani Ikulu hali itaendelea kubaki relatively vilevile. Kama Afrika hatutawekeza kwenye kuzitatua hizi changamoto sita kikamilifu, tusidanganyane kwenye majukwaa ya kisiasa.
 
Umesoma katiba ya wamarekani, rais Hana Kinga. Kuna kesi ya utekaji ilipelekwa mahakama kuu Nini kilitokea lakini kesi Kama hiyo ilipelekwa mahakama kuu ya Kenya maamuzi yalitolewa na hatua zilichukuliwa.
Katiba yetu Ina mapungufu mengi, imewafanya viongozi kuwa miungu watu, polisi wanafanya wanachotaka.
Katiba yetu inahitaji marekebisho kwani hata walioshiriki kuitunga wanajua haifai.
 
wATAnzania wangapi wanajua katiba yao inasemaje? Wakati mmi inailaumu CCM kwa kutumia ujanjaujanja kushinda uchaguzi ninawalaumu zaidi wapinzani kwa kutokuwa tayari mpaka sasa kuweza kupewa nchi kuiongoza. Upinzani wa Tanganyika baaado kabisa. Hawana sera mbadala na watanzania bado hawajutii kuongozwa na CCM mpaka sasa.

Siku zote kama ukiona mtu ametekwa jiulize kwanini yeye ametekwa na wewe hukutekwa. Unataka kusema hakuna watu wanaotekwa kwasababu za mapenzi, mali, kudhulumiana, kuficha ushahidi, au kuwa kibaraka wa mataifa mengine?
 
Back
Top Bottom