Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Simba Queens wameshindwa kufua dafu mbele ya Kenya Police Bullets wakikubali kichapo cha mabao 3-2.
Pambano hilo la nusu fainali lililopigwa kwenye Uwanja wa Abebe Bikila nchini Ethiopia, Simba ilikuwa ikisaka tiketi ya kucheza Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya pili.
Kenya Police ilimaliza nafasi ya pili katika Kundi A ikiwa na pointi 9 huku Simba ikimaliza kinara wa Kundi B ikivuna jumla ya pointi 7 katika mechi tatu, ikifunga mabao 10 na kufungwa mawili tu.
Kinara wa Kundi A, CBE ya Ethiopia ambao ndio wenyeji wenyewe watacheza mechi nyingine ya nusu fainali dhidi ya Kawembe Muslim ya Uganda iliyokuwa ya pili katika Kundi B nyuma ya Simba.
Kwenye kundi hilo Kawembe Muslim ya Uganda ilimaliza nafasi ya pili na pointi sita huku PVP Buyenzi ya Burundi na
fasi ya tatu na pointi mbili na FAD Djibouti ikimaliza mkiani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.