Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Lakini kituo cha tatu cha Citizen kimeendelea kufungiwa.
Kituo cha NTV kimetangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa kimerejesha matangazo kwenye channel zake za kulipiwa, huku KTN News nayo ikirejesha chaneli zake za bure.
Kituo cha Citizen kimeendelea kutokuwa hewani. Vituo hivyo vitatu vilifungiwa baada ya kujaribu kurusha mubashara, hafla ya kujiapisha kwa kiongozi wa Muungano wa Upinzani NASA, Raila Odinga siku ya Jumanne, kama Rais wa wananchi.