MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Hiki kirusi kinabadilisha maisha kama tulivyoyafahamu na kuyazoea, hizi ni enzi za uchizi fulani hivi, naona kwenye habari hapa jamaa wamekamatwa wakinywa pombe kimya kimya maeneo fulani, yaani wote wametiwa lockup na kupelekwa karantini siku 14 kisha baada ya hapo jela itawahusu.
Hamna kingine haswa kwa wale waliozoea kwenda vilabuni ili kukwepa kero za nyumbani, sasa ni mwendo wa kuvumiliana ndani ya nyumba, mnaingia nyote saa moja wakati wa machweo, aidha mnuniane au mchangamkiane, mtajua wenyewe, na pia imetolewa amri hamna mambo ya kutembeleana, msikutwe mumekusanyika kwa nyumba yoyote.
Noma sana sijui itaandikwa vipi kwenye vitabu vya historia.