Kenya sasa ina kila sababu za kukamilisha kipande cha SGR kilichosalia maana Uganda wameamua kujenga SGR 2,700km

Uganda na Kenya hazijawahi kuwa nchi moja, ila zilitawaliwa na mkiloni mmoja yaani muingereza, kutawaliwa na muingereza haina maana ni nchi moja, kwanini husemi Malawi na Zambia ni nchi moja kwasababu zote zilitawaliwa na muingereza?, kwanini Muingereza hakujenga reli toka Zambia hadi Malawi badala yake alijenga Zambia pekee na kuunganisha na Angola ambalo halikua koloni lake?, lengo ni kuunganisha nchi zenye mzigo mkubwa.

Mjerumani alijenga reli ya kati hadi Kigoma, ambayo iliungana na upande wa pili wa ziwa Tanganyaka katika mji wa Kalemii, mizigo toka Zaire ilifika Kalemii na kuvushwa ziwa Tanganyika hadi Kigoma na kuingizwa katika train.

Hizo reli ndogondogo unazozisema hazikujengwa na serikali ya Uingereza bali zilijengwa na wafanyabiashara/Wakulima/Wachimbaji binafsi kwa ajili ya kuhudumia mashamba au Migodi yao, mara tu biashara zao zinapotetereka, hizo reli pia hutetereka, kama ilivyokua reli za mashamba ya katani, machimbo ya almasi kule Mwadui na viwanda mbalimbali ambavyo viliunganishwa kwa njia ya reli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…