JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mfaransa huyo ni Christian Bergeron ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Rubis Energy Kenya ambayo ni kampuni tanzu ya Rubis Group yenye makao makuu Ufaransa.
Mdhibiti wa Nishati, Jumanne ya Aprili 12 aliwashutumu baadhi ya wauzaji wa mafuta kwa kuficha nishati hiyo katika soko la ndani kisha kuuza kwenye masoko ya nchi za nje.
Alisema kampuni hizo zitaadhibiwa kwa kuzuia ujazo wa mafuta wanayoruhusiwa kuingiza Kenya kwa miezi mitatu ijayo.
Makampuni ya Kenya yanauza 65% ya mafuta wanayoingiza kwenye soko la ndani kisha mengine wanasambaza katika Nchi Jirani zikiwemo Uganda, Rwanda na Democratic Republic of Congo.
Kumekuwa na tatizo la uhaba wa mafuta katika wiki za hivi karibuni hali ambayo imesababisha kuwe na foleni nyingi kwenye vituo vya mafuta.
Source: BBC