Kafrican
JF-Expert Member
- Jan 26, 2015
- 7,251
- 7,037
Ni vizuri sana umesema kama tukienda kuuza bidhaa zetu marekani thamani yake itakua hivyo....... Just like tanzania ingeuza bidhaa zake marekani ingepata pesa nyingi zaidi,kama vile mnavyopata hela nyingi zaidi ya utalii....... Lakini hatuko marekani, tuko nchini mwetu na bidhaa nyingi tunajuizia na kununua wenyewe hapa hapa kulingana na inflation rate na thamani ya bidhaa ukitumia pesa za ndani.........kwahivyo Thamani ya hela haendani na kipimo cha uchumi !!!!!Soma vizuri hiyo article utaelewa vizuri, kitu kimoja kizuri umeanza nacho ni kwamba umesema wazi wazi kwamba wewe sio mchumi, kwahiyo sio vizuri kuzungumza kwa undani kama vile wewe ni mchumi.
Thamani ya pesa ya nchi inahusika sana, na ndio kigezo kinachotumika kupima GDP ya nchi, kumbuka GDP ni thamani ya jumla ya nchi ilichokizalisha katika kipindi cha mwaka nzima(Goods and services).
Kenya mwaka Jana mlisema mlizalisha "Goods and Services" vyenye thamani ya Kshs 90trl, lakini kwa ukweli ukichukua hizo "Goods and Services" mkaenda kuviuza Marekani thamani yake ni $60B, yaani Kshs 60trl tu. Yaani bidhaa ambayo Kenya inauzwa Ksh100, thamani halisi ya bidhaa hiyo ni Kshs 70 tu.