Kenya tops again, ranked the second best investment destination in Africa


Narudia tena, kinachowaponza ni katiba, kwamba kwenu huko rais anaamua ujenzi upi anaupa kipau mbele, tumeona hata kwenye kampeni zake anasema wazi bila kuficha kwamba huwa ananyima maeneo ya upinzani maendeleo, sisi kwetu hapa maendeleo yote haya yapo kikatiba zaidi kwa mujibu wa ruwaza ya 2030, kila kiongozi awe wa upinzani au wa serikali hujinadi namna gani atatekeleza hiyo ruwaza.

Kila barabara, reli na vyote vipo kwenye ruwaza, akija rais mpya atalazimika kukomaa nayo, leo hii kuna ujenzi unaendelea tena mambo makubwa na hauskii tukilia kubanwa kwenye mzunguko wa hela maana uandishi wa hii ruwaza uliandaliwa kwa utaalam mkubwa, nyie huko rais ghafla bila kuomba ushauri ananunua mindege kwa pesa taslim na kusabaisha ukata mkubwa vijijini na mitaani.

Mjifunze kuhusisha wataalam wa masuala ya uchumi, acheni hulka ya kukurupuka.
 
Eti mara ya kwanza, unazuga humjui lowasa wa 2015, na ulivyokuwa unamshabikia.
Huyu nae anaishia kama lowasa, tena mwaka huu ndio mteremko
 
Eti mara ya kwanza, unazuga humjui lowasa wa 2015, na ulivyokuwa unamshabikia.
Huyu nae anaishia kama lowasa, tena mwaka huu ndio mteremko

Lowassa yule mzee mlisema alikua mradi, kwanza alikua amechoka hata kampeni zenyewe alikua akiongea machache anaachia, ila huyu dogo jameni kawatoa kamasi hadi mkalazimika kumpiga stop ban ya siku saba ili mumchelewesha, hakupumzika hayo masiku, alikua akienda Kariokoo "kununua" nyanya shughuli inasimama.

Sasa amerejea kwenye shughuli full, naona mipicha amesimamisha shughuli kote kote huko mikoani watu wanamsubiri kwa hamu kila mahali, halafu huyu alivyo na ujasiri, hamtomuweza kwa bao la mikono, atawazingua sana tena yaani dah! Mtu anapigwa risasi 30 na bado anausaka urais, huyu jamaa sijaona kama yeye Afrika, MaCCM mnalo, najua kila mmoja wenu raundi hii tumbojoto, mnajitia mzuka tu wa kuongea ongea ila kiundani mnahaha sana.

Yaani mpaka mumshinde awaachie lazima mtakua mumekipata cha moto. Nahisi baada ya hapo sidhani kama mtakua na yeyote wa kuwabaisha tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…