Kenya tusiwahi kufika huku, siasa za Tz zimeshuka hadhi kiasi cha Corona kuonwa kama kiboko dhidi ya wapinzani

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Yaani watu wamekua personal kiasi cha kiongozi bila kupepesa macho anakusanya umati wa watu na kushukuru Mungu kwamba Corona imempiga mtoto wa kiongozi wa upinzani. Halafu kiongozi mwenyewe kama RC ni mtawala (administrator) maana kwamba yeye hayupo kwenye wadhifa wa kisiasa, ni kiongozi wa wote mfano waziri, haipaswi akawa mbaguzi kihivyo.
Pia viongozi wa chama tawala akina Polepole wanafananisha upinzani na Corona.
Juzi imetolewa orodha ya mataifa ambayo raia wake hawana furaha kabisa, na Tanzania imewekwa miongoni mwa mataifa ambayo watu huchezea mabomu kwao kila siku, ilikua vigumu kumeza hiyo taarifa lakini kama siasa zao zimefikia huku, ni wazi kweli majirani zetu wameharibikiwa.

Kenya pamoja na tofauti zetu, tujiepushe sana kufika huko. Hii hapa video...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…