Kenya tutumie GSU kulinda mipaka yetu kama vile wanavyomlinda UK na statehouse

Kenya tutumie GSU kulinda mipaka yetu kama vile wanavyomlinda UK na statehouse

flyingcrane

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
241
Reaction score
88
Kundi la GSU kitengo cha polisi wa Kenya kina sifa na uzoefu mkubwa katika kulinda amani nchini. Kundi lisilochezea kazi kamwe wanapohitajika, wanaofuzu kuhudumia kundi hili ni wenye masomo ya juu, waliopitia mafunzo ya kijeshi ya hali ya juu ndani na nje ya nchi.

Siku za Rais Moi alitumia GSU kama Jeshi la nchi wakati KDF ilikuwa kambini kwa mazoezi,wao waliilinda nchi kutoka kwa adui wa nje na ndani, mfano mzuri ni wao walipowachafua wasomali wa Northern Kenya waliojaribu kuigawana Kenya ili wajiunge na somali, kuzimisha mapenduzi ya nchi yaliyojaribiwa 1982 na wanajeshi wa Airforce, kupelekwa Zanzibar na kuzimisha fujo kwa siku mbili miaka ya 1961 na kutumika katika jaribio la kuzima ugaidi westgate na kundi lao RECCE ingawa KDF iliharibu oparesheni hiyo, walipambana na jeshi la Uganda wakati wa Idd Amin alipojaribu kuchukua western Kenya na kuwafurusha. Historia tunayo ila hatujifunzi kutokana na historia,tujiulize ni kwa nini Moi aliliamini hili kundi sana kuliko KDF wakati huo.

GSU inahitaji vifaa kama choppers na magari wadili na tukio lolote nchini hasa la kigaidi. kwa sababu ya nidhamu yao ya hali ya juu na kutocheza na kazi tungewapa jukumu la kuilinda mipaka yetu kutoka somalia, TZ, Ug, na Ethiopia sababu kama Kenya police na admnistration police wanashindwa na kazi sababu ya uzembe na kula rushwa basi tuunde kitengo cha GSU kitakachokuwa na kazi ya kulinda mipaka.

Hawa GSU ndio wanaomlinda Rais wetu UK na statehouse hii inamanisha amewaamini na maisha yake kwanini basi asiwaeke wakatulindia mipaka yetu na somalia hasa wakati huu tunapoweka ukuta na vizuizi mpakani mwetu na Somalia.
 
walinde mipaka mbona walishindwa kukamata magaidi wa waste gate,ndio walimuua rogo makusudi huku mombasa, kisha na hao gsu walikiona cha mtema kuni kutoka kwa waislam. mi ni mkatoliki lakini
 
Mwanajeshi ama mlinzi akishindwa kufanya kazi yake vizuri jua shida inatokana na mkuu wake..mzee wa kupika chapati Olelenku ndiye aliyepanga yote hayo, jamaa wako poa kwa kazi lakini orders na mipangilio ndio iliyokuwa mibaya.unaona mambo kidogo yamekuwa nafuu alipoingia Major Nkaisserry
 
nimefurahi sana kuona wakenya sasa mmeamka na kuanza kuitumia JF kujadili maswala yanayohusu taifa lenyu badala kila siku kuonekana mnashinda JF kujibu hoja zinazo anzishwa na watz dhidi ya nchi yenyu.hongereni
 
Back
Top Bottom