joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
MY TAKE; Tony254 Kila tukiwaambia kwamba deni lenu ni kubwa mlikua mkijilinganisha na Japan au USA, Sasa katika orodha ya nchi ambazo zipo kwenye hali mbaya, Japan na USA hazipo.
Jambo lingine ambalo tumekua tukiwaambia ni kuhusu uzalishaji wa chakula, jambo hili wakenya mumekua mkilipuuza kwa muda mrefu badala yake serikali yenu imekua ikiweka nguvu nyingi katika "hi tech sector" na ujenzi wa viwanja vya ndege na Barabara hasa na mijini.
Katika Mambo yanayotajwa kusambaratisha uchumi za Nchi nyingi kwa Sasa ni: 1)Kupanda kwa Bei ya vyakula 2)Deni la taifa 3)Kupanda kwa Bei ya mafuta.
Japo hatuna uwezo wa kudhibiti Bei za mafuta, lakini chakula na deni la taifa ni Mambo ambayo, Kenya, Ethiopia, Ghana na South Africa mnajisababishia wenyewe kwa uzembe wenu.
Kenya mnapaswa kuamka hivi Sasa na kuiwajibisha serikali yenu, msisubiri hadi hali ya Mambo iwe mbaya Kama Sri-Lanka, punguzeni ujuaji mwingi, hali ya maisha na uchumi wenu sio nzuri, ni aibu na ujinga mtupu kwa nchi ambayo uchumi wake unategemea kilimo lakini bado mnatumia pesa nyingi za kigeni kuagiza chakula