Kenya 2022 Kenya: Upotoshaji mitandaoni hatari kwa Uchaguzi

Kenya 2022 Kenya: Upotoshaji mitandaoni hatari kwa Uchaguzi

Kenya 2022 General Election

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kampeni za uchaguzi Kenya zimemalizika rasmi jana lakini wataalamu wa siasa wanahofia juu ya hatari kutokana na taarifa potofu zinazochapishwa mitandaoni na wafuasi wa wagombea wakuu.

Benedict Manzin mchambuzi wa siasa za Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara amesema wafuasi wa Naibu Rais, William Ruto na wale wa Raila Odinga wanasambaza taarifa mitandaoni zinazodai kuwa wapinzani wao wanajihusisha na "njama za wizi wa kura".

Mashirika ya kiraia nchini Kenya na shirika la uangalizi yameonya kwamba taarifa hizo potofu zinahatarisha demokrasia na yameyataka majukwaa ya mitandao ya kijamii kuchukua hatua.

Serikali ya Kenya pia imeanzisha kitengo maalum cha kushughulikia makosa ya uchaguzi na matamshi ya chuki.
 
Hzo sarakasi huwa zipo tuu , na Kura lazima ziibiwe , atakayekufa fresh atakayebaki fresh , mwisho wa sku maisha lazima yaendelee
 
Back
Top Bottom