Kenya: Waislamu wadai ni dhihaka IGP kupiga marufuku maandamano yaliyoruhusiwa na Katiba

Kenya: Waislamu wadai ni dhihaka IGP kupiga marufuku maandamano yaliyoruhusiwa na Katiba

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Taasisi ya Waislamu kwa haki za binadamu(MUHURI) imesema ni dhihaka kwa watu wa Kenya na sheria zake kwa Inspekta generali wa Polisi, Japhet Koome kuhutubia kupitia vyombo vya habari vya Kenya na kusema maandamano yaliyopangwa na Azimio yamepigwa marufuku kwa kiburi.

MUHURI imemkumbusha IG Koome kusoma katiba ya Kenya ambayo inasema sehemu ya maandamano na wajibu wa Polisi. Katiba ya Kenya inasema mtu anayo haki ya kukusanyaka, kuandamana na kutoa waraka kwa mamlaka za Umma.

MUHURI wamesema watamshtaki Koome kwa kuidharau Katiba na kuangalia mauaji ya wakenya wasio na hatia.

Pia wametoa neno la tahadhari kwa polisi wa Kenya, kutotumia vibaya madaraka yao na wajibu wa heshima kulinda maisha na mali za raia wa Kenya ikisema watawajibika kibinafsi kila mtu.

Muhuri1.jpg
Muhuri2.jpg
 
Back
Top Bottom