Chaos Master
JF-Expert Member
- Jul 7, 2021
- 636
- 1,310
Walinzi watatu wa Shule ya upili ya Wasichana ya Komothai Nchini Kenya wamekamatwa kwa tuhuma za kumuua Mwanafunzi wa kiume wa Shule nyingine jirani ya Wavulana aliyekutwa kwenye Bweni la Wasichana la Shule hiyo saa kumi alfajiri wiki iliyopita.
Taarifa ya leo imesema Walinzi hao Joseph Mutahi, Kennedy Muriuki na Mary Achieng waliofikishwa Mahakamani mbele ya Hakimu Mkuu wa Githunguri Victor Asiyo hawakujibu mashtaka yao leo hii baada ya upande wa mashtaka kuomba muda wa siku 15 kuendelea kuwazuia uchunguzi ukiendelea.
Mahakama imeamuru Walinzi hao wazuiliwe kwa muda wa siku saba kuruhusu Polisi kukamilisha uchunguzi dhidi ya mauaji hayo ya Mwanafunzi huyo aitwae Brian Mbage ambaye atazikwa Jumatano hii.
CC: Millard Ayo