Kenya: Waliokumbwa na baa la njaa Kenya wapewa pombe

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Boringo, Kenya. Kampuni ya Chuanshan International, imetoa katoni 20 za pombe iliyotengenezewa China na magunia 300 ya mahindi na katoni 20 za mafuta ya kupikia katika kijiji kinachokumbwa na njaa eneo la Tiaty, Kaunti ya Baringo nchini Kenya.
Wakazi wa kijiji cha Katikit waliokusanyika kupata chakula walishangilia kwa kupiga makofi na vifijo baada ya kutangaziwa kwamba kulikuwa na pombe miongoni mwa chakula cha msaada ambacho kampuni hiyo ilitoa.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chuanshan, Han Ke alisema, aliamua kuweka pombe katika mchango wake wa chakula baada ya kugundua kwamba wakazi wa eneo hilo wanaipenda.
“Wakazi wa eneo hili wanapenda pombe na niliamua iwe sehemu ya chakula cha msaada kwa wanakijiji wanaokumbwa na njaa. Pia tumetoa zaidi ya magunia 300 ya mahindi na mafuta ya kupikia,” alisema Ke.
Kampuni hiyo ilikuwa ikigawa chakula kama sehemu ya jukumu lake la kusaidia jamii ya eneo hilo. Hata hivyo, kizaazaa kilizuka baada ya wakazi kulewa na kuanza kung’ang’ania magunia ya mahindi ambayo yalitakiwa kugawiwa vijiji saba kwa wakazi wenye uhaba wa chakula.
Miongoni mwa vijiji hivyo ni Katikit, Chemusuk, Chemolingot, Kositei, Seretion, Kapturo na Chemisik.
Baadhi ya wakazi pia walichukua madebe ya pombe na kukimbia nayo kwa ajili ya kuyaficha vichakani kuepuka wasipokonywe na wenzao.
Wanawake waliokuwa na watoto wachanga ambao walikuwa wakisubiri chakula pembeni waliungana na vijana waliomwaga mahindi wakitaka pombe.
Baadhi ya wanawake na watoto walianza kuzoa mahindi yaliyomwagika baada ya kugombania na kuvutana huku na kule na wanaume waliokuwapo eneo hilo kila mmoja akidai chakula hicho kilikuwa cha kijiji chao.
Ben Todonyang, aliishukuru kampuni hiyo kwa kuamua kuweka pombe katika mchango wao wa chakula.“Tunashukuru sana kupata pombe katika kijiji chetu. Tumekosa chakula kwa muda na pombe hii itatufanya tuchangamke na kusahau shida zetu,” alisema Todonyang.
Mbunge wa Tiaty, William Kamket ambaye alihudhuria hafla hiyo alisema chakula cha msaada kilichotolewa na Serikali hakikufika eneo hilo kwa sababu ya magari kukosa mafuta.
“Tunashukuru Serikali kwa msaada wa chakula lakini magunia zaidi ya 500 bado yako katika maghala ya Serikali Chemolingot kwa sababu magari hayana mafuta ya kuyasafirisha. Chakula pekee kilichofikia vijiji vinavyokumbwa na njaa ni kile kinachotolewa na wasamaria wema,” alisema.
Hali kama hiyo iliripotiwa kaunti ya Turkana ambapo wakazi wanaendelea kufa njaa licha ya Serikali kutoa chakula cha misaada. Viongozi walisema hakuna magari ya kukifikisha msaada huo kwa wakazi vijijini.



Source : Mwananchi. Newspaper
 
Asante kwa kuwa shabiki nambari wani wa Habari za kikenya
 
Wakipeleka Gongo basi msaada utakua umetimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…