Hongera rais wetu kwa hili, tunashukuru ila vipao mbele havijaandaliwa ipasavyo, wangepewa wenye maambukizi mengine kwanza kisha ifuatiwe na hao wengine kama vile wahudumu.
Sisi wengine tutasubiri zamu yetu maana tuko fit kwa sasa tunadunda mitaani buheri wa afya, mdudu bado anatukondolea macho na kutuchora.
Nina uhakika tena kwa asilimia mia 100% kwamba wenye hela zao matajiri Tanzania watazamia huku kisiri na kupokea chanjo hizi kimya kimya maana kwetu hapa baadhi yetu ni mafisadi wa kupitiliza tusiokua na uzalendo. Akiibuka mtu asiyemkenya na kumwaga hela, anapewa chanjo tu.
Japo nawahurumia walalahoi Tanzania, wataendelea kuimbishwa nyimbo za uzalendo dhidi ya corona huku matajiri wakija Kenya.