Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Baada ya kuchukua bandari zote za Tanganyika kwa mkataba wa kimangungo kwa ahadi kemukemu ambazo hazijaandikwa popote kwamba watazifanya bandari kuwa bora kwa kuvutia mizigo Afrika nzima, wameenda Kenya wakawasainisha mkataba uleule wa kimangungo kwamba watazifanya bandari zao kuwa bora Afrika nzima!
Yani ni sawa na mchezaji anasaini Yanga na kuwaahidi atawafungia magoli mengi balaa msimu huu, baada ya hapo anaenda kusaini tena Simba na kuwaahidi atawafungia magoli mengi balaa msimu huu! Inawezekanaje?
Ina maana hakuna kipengele chochote cha kumbana huyu DP world? Yani kazi ya DPW ni kurundika mashariti tu kwa nchi inazowekeza ila yenyewe hamna kuwekewa shariti hata moja?
Ndiyo maana Prof Shivji akasema kwenye mkataba huu haki zote ni za DP world na wajibu wote ni wa serikali ya Tanzania. Tanzania haina haki yoyote ya kuwawekea hata kipengele kwamba mkishawekeza kwenye bandari za Tanzania basi musiwekeze tena kwenye bandari za washindani wetu kwa terms zilezile na zetu.!
Serikali imepeleka mswada bungeni wa kuifanya sheria ya kulinda rasilimali za taifa iliyotungwa mwaka 2017 na kusainiwa na aliyekuwa rais Hayati Magufuli kuwa isitumike tena ili kuwapa nafasi kampuni la DP world kuchukua bandari zote za Tanganyika na kuziwekeza kadiri watakavyoona inafaa.
Ikumbukwe wakati sheria ya kulinda rasilimali za taifa inatungwa waziri mkuu alikuwa ni huyu Kassim Majaliwa , naibu spika alikuwa ni Dk Tulia, makamu wa rais alikuwa ni Samia Suluhu, waziri wa sheria alikuwa ni Mwigulu Nchemba, na wabunge waliopitisha bungeni ni hao hao wa CCM!
Watu ni walele na chama ni kilele waliotaka na kuona kuna umuhimu wa kutunga sheria ya kulinda rasilimali za taifa ,lakini sasa ni haohao hawaitaki tena hiyo sheria, wanaona hamna haja ya kuwa na sheria ya kulinda rasilimali za taifa.!
Je, wakati wanaitunga na kuipitisha hii sheria waliipitisha kwa kuwa walikuwa na uchungu wa rasilimali za taifa kutoka moyoni? Au walipitisha tu kwa sababu tu rais alikuwa ni Magufuli?
Tunaposema Magufuli alizungukwa na wanafiki kutoka kichwani hadi miguuni mtuelewe jamani.