Kenya yachoma hifadhi yake ya Pembe za Ndovu na Faru zenye thamani zaidi ya Tshs Billn 450

Kenya yachoma hifadhi yake ya Pembe za Ndovu na Faru zenye thamani zaidi ya Tshs Billn 450

BUSAMUDA

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2014
Posts
612
Reaction score
358
Rais wa Kenya tarehe 30/04/2016 ameidhinisha uchomaji wa Pembe za Ndovu Zenye thamani ya zaidi ya Tshs bill 300 na Pembe za Faru Zenye zaidi ya Tshs Bill 150.

Sherehe hizi zilihudhuriwa na rais wa Uganda Yoel Museveni na viongozi mbalimbali Africa.

Zinakadiliwa kutoka kwa zaidi ya tembo 8,000

Pembe za Faru zimetoka kwa zaidi ya Faru 343

Akiongea na CNN mhifadhi Richard Leakey anasema katika Dakika 15 duniani tembo 1 huuawa na majangiri.

John Scanlon anasema huu ni ujumbe Kenya inatuma duniani kuwa Kenya itapambana na biashara hii haramu ya wanyama pori."

Now it's Tanzania turn to burn its ivory stock.

Historic ivory burn covers the sky in smoke and ash
Millions of dollars of tusks, horn burn in Kenya - CNN.com
 
Siwezi kuzichoma aisee, why should I lose all those billions and end up looking for loans and grants of the same amount somewhere else... I'm sorry I can't
 
Yaani nichome hela?halafu kesho niende nikakope tena hela? Hapana aisee
 
Usiochoma ina maana utauza au kubadilisha matumizi na matokeo yake wewe mwenyeww utaendelea kuchochea na kuhamasisha soko haramu la pembe za ndovu na kusifu kazi ya majangili,,kwahiyo ujangili utaendelea na tembo kuzid kuuawa
Big up to kenya aiseee,piga vita kutomomeza ujangiri
Kwa mujibu wa salim kikeke BBC swahil news, 65% ya tembo wameangamizwa ukanda huu,ujangil ukiendelea itafika kipindi vizazi vijavyo wataona kwenye picha tu kulikuwa na mnyama anaitwa tembo
 
magufuri asiige hyo mbinu mana niyakipuuzi. abuni njia nyingne ya kupambana na hilo janga.
 
Kwa Tanzania hii ni ndoto labda kizazi cha Mwaka 3000 kinaweza fikiria kuchoma fedha hiyo
 
kinana 1 baridi akiona hiyo weza kuwa kichaa.

swissme
 
mmmh sisi hatuwezi choma!
Mpaka sasa imeshashindikana kuziuza Pembe zilizohifadhiwa pale keko. Hakuna jinsi ni bora tuzichome kwa kuwa gharama za kuzihifadhi zimeshakuwa kubwa na pia ni majaribu kwa wale waliopewa mamlaka ya kuzihifadhi.
 
Naomba kujua tofauti kati ya Pembe za Ndovu na Meno ya Tembo
 
Tatizo lingine la watu weusi kutaka kuwafurahisha wazungu,, una pembe za ndovu zenye thamani ya tsh billioni 450, taifa lako masikini kutwa kucha bajeti haitoshi na hizi pembe tayari ndovu wakutosha wameshakufa na hazina effect yoyote kwa binadamu hao wanaoziitaji yaani kwa kifupi ukiziuza kwa wachina haziwezi kuja kudhuru watu wako... Uza hizo pembe hizo hela fanyia biashara na faida itumie kuimarisha kulinda mbuga tembo wengine wasife...
 
Siyo watu weusi ila ni watawala weusi.
Nina amini kuna wengi wenye fikra chanya ila hawako katika ngazi za maamuzi
 
Tatizo lingine la watu weusi kutaka kuwafurahisha wazungu,, una pembe za ndovu zenye thamani ya tsh billioni 450, taifa lako masikini kutwa kucha bajeti haitoshi na hizi pembe tayari ndovu wakutosha wameshakufa na hazina effect yoyote kwa binadamu hao wanaoziitaji yaani kwa kifupi ukiziuza kwa wachina haziwezi kuja kudhuru watu wako... Uza hizo pembe hizo hela fanyia biashara na faida itumie kuimarisha kulinda mbuga tembo wengine wasife...
WARNING: usitumie ubongo wako kama pambo la ndani!
 
Kwahiyo ukichoma ndo umepiga vita ujangiri?
let's think guys tunakimbilia kucomment sana
kwa mfano: huwezi ukazuia watu kutupa taka sehem flani wakati unamwaga taka palepale.
ndo sawa na kupiga vita biashara ya pembe za ndovu (ndo inayoleteleza ujangili) huku wewe ndo supplier mkubwa.
 
Wengi wamelaani kuwa kuzichoma sio suluhisho la kuhifadhi. Ni vyema zingeuzwa na mapato yake yatumike kuboresha uhifadhi wa wanyama hao.
 
Back
Top Bottom