Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Msemaji wa Serikali ya Kenya, Isaac Mwaura amesema kuwa taifa hilo limepoteza zaidi ya pesa za kenya bilioni 6 (zaidi ya bilioni 123 za Tanzania) kutokana na wimbi la maandamano yaliyoshuhudiwa katika mwezi uliopita.
Katika taarifa kwa wanahabari Mwaura ameeleza kuwa nchi imepoteza mabilioni kutokana na kufungwa kwa biashara wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumanne na Alhamisi tangu Juni 18, 2024.
Ameongeza kuwa biashara kadhaa pia ziliporwa na mali kuharibiwa na wahuni waliojipenyeza katika maandamano hayo ya amani na kusababisha fujo.