Kenya yaripotiwa kufungia mtandao wa Telegram ili kuzuia udanganyifu kwenye mitihani

Kenya yaripotiwa kufungia mtandao wa Telegram ili kuzuia udanganyifu kwenye mitihani

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Shirika la Netblocks, hivi karibuni limeripoti kuwa, kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imezuia upatikanaji wa app ya Telegram kwa wateja wake walioko nchini Kenya.

Netblock imedokeza kuwa Safaricom ambayo ndio kampuni kubwa ya mawasiliano nchini Kenya – imezuia upatikanaji wa Telegram nchini humo ili kupunguza kiwango cha udanganyifu katika kipindi hiki ambacho mitihani ya kumaliza elimu ya Sekondari hufanyika (KCSE)

Netbloc.png


Kwa nchini Kenya, Telegram imedaiwa kutumika sana katika kuvujisha na kusambaza mitihani na kama ilivyokuwa kwa mwaka 2023, serikali ya Kenya wala Safaricom hawajatoa tamko rasmi kuhusu hatua yao ya kufunga mtandao huo mwaka huu.

Soma pia:
UN watoa ripoti mpya kuhusu app ya Telegram. Yadai inahusika katika kuwezesha makundi ya uhalifu na shughuli haramu!

Inakadiriwa kuwa mwezi Novemba 2023, Kenya ilipoteza takriban dola milioni 27.02 kutokana na kufungwa kwa Telegram, ambapo wafanyabiashara walikadiriwa kupoteza wastani wa dola milioni 4.2 kila siku.

Kando na kipindi hiki cha mitihani, Safaricom pia ilitajwa kuzuia na kukatiza huduma za mtandao kwa muda wakati wa maandamano yaliyotokea kwenye miji mikuu ya Kenya mwezi Juni, ambapo vijana walijitokeza mitaani kupinga ongezeko la kodi kwenye muswada maarufu ulioitwa FInance Bill

Source: Netblock, Hypertext
 
Kwa hiyo tuseme Vodacom au Airtel wanaweza kuzuia upatikanaji na utumiaji wa Telegram Tanzania? Ninachojua Mamlaka za mawasiliano kama TCRA ndizo zina huo uwezo.
 
Kwamba pepa likivuja linasambazwa kwa haraka kupitia telegram??
Wanazuia usambazaji
 
Wafunge internet yote kabisa, Maana njia za kusambaziana nyaraka mtandaoni ziko nyingi sana.
 
Back
Top Bottom