Kenya yatengeneza Setilaiti yake ya kwanza

Kenya yatengeneza Setilaiti yake ya kwanza

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.

Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitenengeza chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.Setlaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo.

Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema setilaiti hiyo ni ya umbo la mchemraba na ina ukubwa wa sentimita 10 mraba - hujulikana kama nano-setilaiti.Japan ilitoa ufadhili na jukwaa la kuitengenezea lakini ni Wakenya wenyewe walioitengeneza.

Setlaiti hiyo itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) mnamo mwezi Machi na kuzinduliwa rasmi kuizungukza dunia na roboti mwezi mmoja baadaye.Hatua hiyo itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa sita barani Afrika yaliyo na setilaiti zinazoizunguka dunia.

Kundi la wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi walioitengeza walikuwa kundi la kwanza kufaidika kutokana na mradi wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na shirila la anga za juu la Japan unaolenga kuzisaidia taasisi za elimu kutoka mataifa yanayostawi kutengeneza setilaiti zao.

Chanzo: BBC
 
Hio Setlite ina ukubwa wa Sentimita 10 za Mraba? Inamaana ina ukubwa wa Kibiriti?
Hio ni kubwa sijawahi kusikia kama Satelite kama hio inaweza kurushwa na ikaingia kwenye Orbit na kufanya Safari kuzunguuka Dunia. Watu wa Pwani husema taire mkuu
 
Hongera Kenya. Hata ss Tz tupo na huo mpango lkn ngoja kwanza awamu hii tusambaratishe hawa upinzani alafu tumalizie chaguzi theni tutaandaa bajet ya kukamilisha mpango huo kwa hiyo Kenya msijisifu sana twawanusa kwa nyuma [emoji53][emoji53][emoji53][emoji53][emoji53][emoji53]
 
1. Tukimaliza kusambaratisha kabisa chama fulani, tunaweza kufikiria kuwezesha mambo hayo.
2. Serikali ina mahela! Imeweza kujenga SGR kwa fedha zake.
3. He hawa wachawi hawawezi kuruhusiwa kupeka ungo huko majuu, kisha tukawaita hao BBC?
 
Hio Setlite ina ukubwa wa Sentimita 10 za Mraba? Inamaana ina ukubwa wa Kibiriti?
Hio ni kubwa sijawahi kusikia kama Satelite kama hio inaweza kurushwa na ikaingia kwenye Orbit na kufanya Safari kuzunguuka Dunia. Watu wa Pwani husema taire mkuu
Nadhan kadri teknolojia inavyokuwa inapelekea kuwa na devices ndogo , isiyochukua nafasi, power mdogo(solar au battery) au cost pia. Tukubali tu kwa hili wamepiga ka hatua
 
1. Tukimaliza kusambaratisha kabisa chama fulani, tunaweza kufikiria kuwezesha mambo hayo

Baada ya kutengeneza tunakwenda kwa jirani kuuliza tuitumie kwa shughuli gani ati!!
 
Nadhan kadri teknolojia inavyokuwa inapelekea kuwa na devices ndogo , isiyochukua nafasi, power mdogo(solar au battery) au cost pia. Tukubali tu kwa hili wamepiga ka hatua
Tunakubali kuwa ni hatua mzuri sana na tunawapongeza, kaini unaposoma habari na wewe icheki kwanza usahihi wake. Satelite ina hitaji Nafasi ya kuweka mitambo humo ndani kwa ajili ya uchunguzi pamoja na kutuma Report duniani, wataiweka wapi. Tatu chombo chenye ukubwa huo hakiwezi huruka anga za juu, ni chesi sana na kitachukuliwa na upepo na kitapotea
 
Mimi hapo kwenye ukubwa mbona kama sijaelewa aisee!

Mana ile ilirushwa miaka ya 1960's ambayo ndo mpaka saivi inatumiwa nilisikia ina uzito ya tani 63 kama sikosei... je ukubwa wake!?
 
Wazee wa manunuzi ya wabunge na madiwani na mabalozi wa nyumba kumi kusanya kodi kwa nguvu unampelekea Mtulia na familia yake.
 
Mimi hapo kwenye ukubwa mbona kama sijaelewa aisee!

Mana ile ilirushwa miaka ya 1960's ambayo ndo mpaka saivi inatumiwa nilisikia ina uzito ya tani 63 kama sikosei... je ukubwa wake!?
satelite zimezidi kuwa ndogo,lakini perfomance ni zaidi ya hiyo ya tani 60,

sikuhizi kuna satelite za kilo moja,kila tano etc
 
Back
Top Bottom