joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Marubani wanafunzi kutoka Afrika Kusini watua KIA baada ya kuzuiwa Kenya
Marubani wanafunzi kutoka Afrika Kusini watua KIA baada ya kuzuiwa Kenya
Ikionekana kama ni tukio la Kenya kulipiza kisasi kwa South Africa kukataa kuondoa viza kwa wakenya kuingia SouthAftica, jambo ambalo Kenya imekua ikiliomba kwa miaka mingi.
Kenya imeamua kujitoa muhanga ili kutunisha misuli dhidi ya South Africa, baada ya kukataa kuwaruhusu marubani wanafunzi toka South Africa, wanaoelekea Cairo, Misri kwa kutumia ndege ndogo waliyoitengeneza wao wenyewe, kutua JKIA kwa muda, hivyo kulazimika kutua KIA toka Zanzibar.
Kwasababu ndege yao ni ndogo, haina uwezo WA kusafiri umbali mrefu bila kutua ili kujaza mafupa, kwasasa wapo KIA ili kuangalia njia ipi wanaweza kutumia ili kufika Cairo. Ninakumbuka ni juzi tu Kenya ilikua inafurahia mkataba wa Africa free Airspace, ni jambo la kushangaza kusikia kwamba Kenya ndio nchi ya kwanza kuanza kukiuka mkataba huo hata kabla haujaanza, Tusibiri majibu toka kwa Ciryl Ramaphosa.