Kenya yazidi kupaa "Ease of doing business", hamjakoma bado

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Dah ila Rwanda wale watu wanajituma, wana rais asiye mzembe, bado wanaongoza kwenye hili, ndio tatizo haupewi vyote aidha upewe ubongo na kunyimwa raslimali au upewe raslimali unyimwe ubongo.

Hata hivyo Kenya inazidi kuchana mbuga tena kwa kasi ya ajabu, majirani zetu wengine tumewapiga double double, majirani mnatuchelewesha sana kwa mlivyo wazembe sijui mfanywe nini muamke, maana binadamu akizungukwa na wazembe hata yeye hujikuta akizembea maana lazima awaburuze au wamburuze.

Rwanda 76.5
Kenya 73.2
Uganda 60
Tanzania 54
Burundi 46.8
Sudan Kusini 34.6

https://www.doingbusiness.org/content/dam/doingBusiness/media/Profiles/Regional/DB2020/SSA.pdf
 
Hehe.. hii inasaidia kuongezeka kwa dola milionea eh?
 
Ni rahisi sana kufanya biashara ya ufisadi Kenya. Haijalishi hata kama nikupiga pesa ya wagonjwa wa COVID.. Bora usajili kampuni yako mwezi mmoja na uwe na Connections na wanasiasa.

Tanzania ni vingumu sana kupiga hela, hata mifisadi iliyo komaa na kujua system wanajikwaa kwa mwamba JIWE
 
Urahisi wa Kufanya bizz ni pamoja na maslahi kwa taifa sio kulegeza masharti watu wageuze kwenu shamba la bibi wapige hela nyie mnabaki na manyoya.
 
Hilo tulilitegemea mbona kitambo tu, si mlipewa mihela ya corona.

Tushajua Kila ripoti zenye harufu ya ubeberu mtakua mnaongoza
 
Urahisi wa Kufanya bizz ni pamoja na maslahi kwa taifa sio kulegeza masharti watu wageuze kwenu shamba la bibi wapige hela nyie mnabaki na manyoya

Huwa nakuona Mtanzania ambaye hushirikisha ubongo wakati unajadili hoja, pitia vigezo vyote vinavyoangaliwa, amin nawaambieni haitokuja siku ujiweke kwenye ugomvi na wana biashara, wakulima na wawekezaji kisha utegemee kupaa, mwisho wa siku hata ujenge miundo mbinu inayonyoosha hadi kwenye mawingu ila hao hao ndio utategemea wayatumie ili kukuza uchumi wako.

Kenya hapa tunajaribu kila namna kuweka mazingira mazuri kwa wana biashara, kero zipo tu kwenye ufisadi, kama kuna kitu hunikera kwenye nchi hii ni ufisadi, aki yaani huwa natamani kubunwe kikosi cha wasiojulikana wanakuondolea mbali ikigunduliwa na kubainika umepiga ufisadi wa kiwango cha juu.

Nahisi ndio namna Kagame hufanya kwake huko, rais Uhuru ametufeli sana kwenye hili la ufisadi, huwa namuunga mikono kwenye mengi tu lakini hili la ufisadi kazembea, uzuri Kenya hapa tuna uhuru wa kusema, sio kama Tz mataga ni mwendo wa mapambio kwa rais kweye kila kitu.
 
Shukrani, Hapa Tz kwa sasa na haya mambo ya uchaguzi bado mambo hayajatulia kabisa,Hizi sintofaham zinazoendelea utafika wakati zitapita tu Naamini!!

Ufisadi ndio umemaliza nakuhakikishia enzi ya Kikwete angekua mkali tungekua mbali sana kwa sasa...Ufisadi utawapeleka pabaya kuweni serious
 
Comment ya pili nimeikubali maana haujaweka double standards Ila ya kwanza kabla ya kuiandika ungeenda kunya kwanza.
 
MK254,

Anzeni kwanza na hii hapa ndiyo mje kutuonesha easy of doing business.
If easy of doing business do not benefit local is a useless information.

 
Tangia mzee wa mikwara atinge ikulu Tz imekuwa ikiporomoka kweli kweli kwenye rank kama hizi na eti kuna wanakwaya humu wanadhani ni sifa. Upumbavu ni kujua kwamba ease of doing business inawahusu wageni tu. Hapo hapo mnakomoana wenyewe kwa wenyewe na kurudishana nyuma kibiashara kisa red tape, protokali za kijinga, 'visheria' vya kipuuzi na uzembe uzembe.
 

Usiongee vitu usivyojua budaa, awamu hii ndio inaongoza kwa kuondoa kodi zisizo rafiki katika biashara na kuondoa urasimu sana. Ndio maana saiv mapato yameongezeka sana kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, madini n.k.. ni kutokana na kuondolewa kodi sumbufu. Saiv kuanzisha kiwanda au biashara ni fasta tu hakuna tena bureaucracy wala red tape.

Halafu usishanguilie hiyo report sana maana hata WB wenyewe wameshakiri ina makosa hivyo itafanyiwa kazi upya kwa kuchukua data upya katika nchi mbali mbali.

Release of World Bank 'Doing Business' report halted over fudging of data
 

Nacheck check hizo siasa zenu za uchaguzi yaani zinahuzunisha sana, hapa Afrika siasa hupunguza uzalendo kwa idadi kubwa sana ya wananchi, hapa kwetu huwa natamani kama kuna namna ya kukwepa uchaguzi maana ndio kipindi nchi hugawanyika noma, kwamba hata aliyeshinda anajikuta hana hamu na ushindi wake. Elimu inapaswa kutolewa kwa wananchi Afrika wafahamu maana ya uchaguzi nini, atakayeshinda ashinde kwa njia za haki na aliyeshindwa ahamasishe uzalendo kwa wafuasi wake ili taifa lote lisonge mbele, ila huwa knyume, unakuta mamlioni ya wananchi wanabaki kuwa na hasira, wengi wakitamani hata kuhusika kwenye uhaini.
 
Hujaeleweka. Uchaguzi wetu utakuwa wa amani. Wewe fuatilia kwenye vyombo vya habari.

Also usiifananishe Tanzania na mambo ya kijinga.
 
can you listen to yourself speak? corruption is one of the blockers of ease of doing business..
if TZ is not corrupt then means your processes are blocked by bureaucracy
 
Hujaeleweka. Uchaguzi wetu utakuwa wa amani. Wewe fuatilia kwenye vyombo vya habari.

Also usiifananishe Tanzania na mambo ya kijinga.

Siwaombei ukosefu wa amani, ila mataga mjifunze kitu, acheni kiburi mfahamu hamna kitu kibaya kama mamilioni ya wananchi wenye hasira na wanaohisi kukandamizwa kwa uhuru wao wa maamuzi, hata kama hawatatokea barabarani kuomba haki ila ile tu hasira za ndani kwa ndani ni kitu kibaya sana.
Huku kwetu hata nikiwa mlengo wa serikali lakini itokee mgombeaji niliyempigia kura ametangazwa mshindi huku kukiwa na mashaka na uwalakini mwingi hususan magoli ya mikono kama yale yenu, huninyima amani sana hata bila ya fujo.
 
Sasa riwaya yote unamwandikia nani!?
Yaani wewe utufundishe namna ya kuishi!?

Hizo ni hisia zako tu, kutokana na negative minds about Tanzania.

Tumeanza multipartism since 1992 so you have nothing to tell us.
Hizo bad wishes utabaki kuzisikia tu. Mkijaribu kutaka kujiingiza kwenye uchaguzi wetu. Tutawajibu kwa nguvu zote.
 

Unajua nini maana ya multiparty system au unatumia maneno kisa unayaskia.
 
Unajua nini maana ya multiparty system au unatumia maneno kisa unayaskia.
Umechemka kijana. Foundation ya Tanzania ni kubwa mno.
Tanzania mwaka huu vipo vyama 20 vimeweka mgombea urais.
 
Umechemka kijana. Foundation ya Tanzania ni kubwa mno.
Tanzania mwaka huu vipo vyama 20 vimeweka mgombea urais.

Akina nani hao sijui eti Lipumba??? Sema mtapata ushindani mkali sana kwa mwanasheria, jamaa ana ujasiri kinyama, licha ya kumuondoa kwa marisasi bado kageuza, na isitoshe katupia mapingamizi ambayo mliyapiga chini bila kuipangua kisheria.
Halafu ameomba mdahalo japo najua hamuwezi kuthubutu maana jamaa yuko balaa sana.....amehamasisha muamko mpya kwenye mlengo upinzani lakini mlivyo, mnawaengua wagombeaji majimboni na wagombeaji wenu kupita bila ushindani.
Inatia moyo kuona Afrika bado kuna majasiri kama huyo jamaa, akina Mandela wa leo, ipo siku tutaaga siasa mbovu na umaskini.
 
My Friend hujui siasa za Tanzania. Unachotakiwa ni kukaa kimya ujifunze.
Huenda umri wako ni mdogo. Sidhani kama unafikisha umri wa miaka 30.

Uchaguzi ulikuwa wa moto ni mwaka 1995 mpinzani akiwa Mrema, na Mwaka 2015 Mpinzani akiwa Lowassa.

Jifunze na uzijue siasa za Tanzania. Wewe subiri utaona. Leo CHADEMA wameanza kampeni. Kesho CCM.
So uwe mvumilivu tu maana kampeni ni miezi 3.

Nadhani kwa kipindi hiki utajifunza mengi maana umeshakuwa mtu mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…