Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Gavana wa Kajiado Joseph Lenku amefunga kabisa uuzaji wa Ng’o,mbe katika kaunti hiyo kutoka Tanzania kutokana na visa vya maambukizi mengi zaidi yanayoripotiwa nchini humo.
Lenku ametoa amri hiyo baada ya kufanya ziara eneo la Loitoktok ambapo alikuwa anasambaza barakoa kwa wenyeji .
“No Tanzanian cattle will be allowed in Kajiado livestock markets in Namanga, Loitokitok, and Shompole border points. We have completely locked the border,” alisema Lenku.
Wakaazi wa kaunti hiyo aidha walikuwa wamemkashifu Lenku kwa kutozuiya uuzaji wa Ng’ombe eneo hilo kutoka Tanzania kwa hofu ya kuambukizwa Corona.
Kisa cha kwanza cha virusi hivyo kaunti ya Kajiado kiliripotiwa Machi 6 na wakaazi wa eneo hilo walityarajia kuwa huenda gavana huyo angefunga kabisa mipaka kati ya Kajiado na Tanzania.
Wiki jana hatua ya maambukizi kuongezeka katika taifa jirani la Tanzania ilitia hofu kwa idadi kubwa ya wakenya haswa wanaoishi karibu na mipaka ya mataifa haya mawili kama vikle Loitoktok,Namanga ,Shompole na karibu na ziwa Natron.