Kenyan MPs award themselves Sh 2bn in secret deal....President Kibaki rejects it!

Kama Angekuwa Dr Dhaifu angewaongezea asilimia 200
Hahahahaaa, lakini naona sasa hapa kwetu kila kitu tumekuwa tunaki politisize hata yale masuala ya msingi.

Walimu walipodai maslahi hapa kwetu waliambiwa ni siasa na pesa haziwezi kupatikana, madaktari hali kadhalika ikasemekana wanasukumwa na wanasiasa fulani wakaishia kufukuzwa kazi (baadhi yao)

Wabunge wakaongezewa kwa madai kwamba maisha yamekuwa magumu...........Dah comedy hizi za nchi hii!
 

Hiii safi sana. Lakini mkuu hii pia ilitokana na nguvu ya umma. Jana watu wameandamana hadi kwenye viunga vya bunge kuwasuta wabunge. Naona na Kibaki akasoma alama za nyakati akaamua kufutilia mbali upandishaji wa mishahara/posho. Inapofika kwenye masuala ya hela humsikii Raila, Orengo, Kenyatta, Mudavadi, Ruto au Kalonzo. Nilimsikia tu Martha Karua akipiga kelele wengine kimya.

Wanasiasa wote inapofika suala la kuwanyonya wananchi basi huungana na kuanza kunyonya.
 
kikwete hakuchaguliwa na watanzania aliiba kura. Kibaki naye aliiba ila yeye ana akili kidogo

Kumbe tatizo la Rais wetu ni upeo finyu ukilinganisha na Rais wa Kenya?. Sasa mbona bado anapigiwa debe na watu wengi kuwa serikali yake sikivu?. Au usikivu huo ni exclusive kwa wananchi masikini wa Tz?. Nadhani bado kuna kitu kichafu kimefichika kwenye mfumo mzima wa utawala utokanao na ccm.
 
Mkuu hapa ukiandamana utauawa na polisi...............na Ripoti itasema hukutii amri halali
 

tatizo hata hao wabunge wa upinzani tunao wategemea waliungana na serekali na sijasikia hata mmoja akipinga au akikataa nyongeza.
Hapo ndipo utapojua uongo na unafiki wa wanasiasa.

Siku zote maslahi yao kwanza then ya wengine, ni wataalam wa kusema wasiyotekeleza.

Utashangaa wanailaumu serekali kwa kutumia magari ya kifahari wakati wao pia wanayatumia na sijawahi kusikia hata mmoja akikataa na kutaka gari la bei nafuu na linalokunywa mafuta kidogo.

Kwa tanzania yetu, bado sana kuondoka kwenye umasikini.
 

umenena vyema sana mkuu, hata hapa kwetu ni hivyohivyo.
Walipopandishiwa mshahara sio ccm wala cdm waliokataa nyongeza.

Hili linadhihirisha Bado wanasiasa wengi hawana nia ya dhati ya kuondoa umasikini katika nchi yetu.

Tutaendelea kupiga kelele sana lakini tusipo badilika kuanzia ndani ya mioyo yetu mambo yatakuwa yaleyale.
 

Mkuu kwenye siasa hayo unayoyasema ni dhambi kuu! Wote lao moja
 

Kimbunga, Raila alipinga sema wewe hukumsikia tu. Fuatilia ukurasa wake wa twitter, alilipigia kelele jambo hili hata kabla Kibaki hajakataa!
 

Kenyan lawmakers are already some of the best paid on the continent

Civil society groups took to the streets on Tuesday as pressure continues to mount on President Mwai Kibaki not to assent the proposed MPs pay perks.

The youthful demonstrators in a statement read by Roy Ogola say if the bill goes through it will be an extra burden to the already overtaxed ordinary Kenyan in these harsh economic times. The lobby groups said the move by the MPs violates the constitution.

Last Thursday the MPs sneaked amendments to the Finance Bill 2012 and voted it to award themselves the 2 billion shillings gratuities at the end of their term. Each MP is set to receive 9.3 million shillings.

"It is totally ridiculous for the MPs to award themselves such an amount of money," said Morris Odhiambo, who helped organise the demonstration.

The demonstrators, waving placards with messages such as "MPs are thieves" and "greedy hyenas", marched through central Nairobi to parliament.

"We want them to know that the public mood is against this unjustified increment," said Robert Alai, another of the organisers. "How come our teachers had to strike for three weeks to get a salary hike, yet within a single sitting the MPs could easily increase their remuneration," Odhiambo said. "So where is the two billion shillings going to come from?"

The proposed golden handshake - which must still be ratified by President Kibaki - comes after the Finance ministry has already proposed tax rises to pay for public sector wage increase demands.

Rights groups, including Transparency International and the Kenya Human Rights Commission, said in a joint statement the move was "extremely disturbing" and broke constitutional rules.

The statement called on Kenyans to let lawmakers "know that they are not willing to foot the cost of their greed."
Prime Minister Raila Odinga has said he is "against the MP's gratuity bonus."

Kenya is due to hold in March 2013 the first general election since deadly post-poll violence four and half years ago.

Kenya's government was propped up by some $270 million in foreign aid in 2010-2011, according to official figures, and faces a $1.6 billion deficit in the year ahead.
 
Kikwete mnaumuonea buree; wabunge Kenya walipwa zaidi ya wabunge wa Marekani; kwenye huo mswaada pamoja na kujiongeza mishahara, bado kuna kipengele ukiwa mbunge ukishindwa utaendelea kulipwa kwa muda wote wa maisha yako; yaani jamaa ni noma
 
By PPS | October 09, 2012


President Mwai Kibaki has declined to assent to the amendment to the Finance Bill (2012) that was passed by Parliament on Thursday October 4th, 2012.

The amendment awarded MPs hefty severance allowances.

The President objected to the amendment on the grounds that it was first unconstitutional and that in the prevailing economic circumstances in the country, it is unaffordable.

The President said that coming shortly after the increment of salaries for teachers and doctors, the severance pay for Parliamentarians would lead to an unsustainable wage bill at a time when the country requires massive resources to implement the new constitution and meet other competing demands in the economy.

Earlier in the day, members of the public held protests along city streets protesting the move by MPs to award themselves Sh2b in bonus when their term in office expires.

In the meantime, the Head of State has assented to the amendment in the electoral laws extending the period to January 4, 2013 during which Members of Parliament should have chosen the political party on which to seek nomination and contest a political seat in the forthcoming general elections.
 
Kuna anayefahamu kiasi wanachopata wabunge wa Kenya kabla ya kutaka kuongezewa?
 
Mkuu coz nao ni wabunge tu yaani kuwa mule ni kama kuna ka very contagious ugonjwa hivi kanawakumba wooote
 

Yesterday people demonstrated, and some are still planning to demonstrate on Saturday, occupy parliament will be the slogan and hopefully we will manage to kick the thugs out of parliament come 2013. A people's revolution is in the making, we are just waiting for the leaders.
 
Kuna anayefahamu kiasi wanachopata wabunge wa Kenya kabla ya kutaka kuongezewa?

Sina hesabu kamili lakini walichotaka kuongezwa sio mshahara bali ni kama retirement package. Walifanya hila kama hizo na kuongezea mishahara yao kutoka takribani ksh.250,000 hadi takribani ksh. 850,000(multiply mara kumi na tisa upate kwa pesa za Tanzania)
 
Kikwete mnaumuonea buree; wabunge Kenya walipwa zaidi ya wabunge wa Marekani; kwenye huo mswaada pamoja na kujiongeza mishahara, bado kuna kipengele ukiwa mbunge ukishindwa utaendelea kulipwa kwa muda wote wa maisha yako; yaani jamaa ni noma
kama wabunge wa kenya wanalipwa zaidi,basi ndio halali kwa wabunge wa Tanzania kujiongezea mishahara na posho hali watumishi wengine wa umma pamoja na walimu na madaktari ambao kipato chao ni kidogo wakipuuzwa.Ifike kipindi sasa viongozi wetu wamwogope Mungu na waache uwongo na waone aibu.siku za nyuma tuliambiwa kuwa serikali imeamua kukomesha suala la malimbikizo ya malipo ya watumishi wake,cha ajabu leo mamia ya walimu ktk halmashauri ya jiji la mwanza wanasotea kulipwa malimbikizo ya mishahara yao kwa miaka 4 sasa bila mafanikio wakati wabunge wakikohoa tu wanalipwa.wafanya biashara na wakulima hivi sasa wana hali ngumu, lkn serikali imeamua kuwajali zaidi wabunge kwa kigezo kuwa Dodoma kuna maisha magumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…