Wadau hii ishu ya wakenya kuja bongo kuchukua/kununua mazao ya kilimo kama vitunguu, maharage, mahindi na kupeleka Kenya kufanyia package na kuuza Ulaya inaniumiza sana. Ni kama vile wabongo tumelala kifikra.
Ni mda sasa tulime wenyewe, tufanya good packaging na kutafuta soko nje wenyewe ili tuweze kupata faida Nzuri zaidi na sio kulima bidhaa na kutegemea Wakenya kununua wakati tunaweza fanya mambo makubwa zaidi wenyewe.
Don't get me wrong. Let's discuss this. Maana hawa jamaa wanakuwa tishio sasa. Tanzania nzima wamejaa wananua mashamba na maeneo makubwa na kujigamba. Hadi wanaigeria nao wapo!
Wenye connection na details za soko la nje bara ya Ulaya mwageni details hapa tuanze supplies ya mazao ya Kilimo
Mkuu Kingdom, kiukweli, sisi Watanzania tuna tatizo, tukubali tukatae, we are not aggressive and serious enough!.
Fursa za soko la AGOA kwa nchi za Marekani zilipoletwa, nchi za Afrika ya Mashariki, ziliwekwa block moja!. Wamarekani wakaja kuendesha semina za bidhaa wanazotaka, nyingi zikiwa ni bidhaa za asili, handcrafts na mapambo zikiwemo batik, namna ya packaging, branding na export procedure, wafanyabiasha wa Tanzania wakajitokeza kwa mamia!.Wakatoa miezi sita kwa wafanya biashara wa Tanzania, Kenya na Uganda kupeleka sample US ili wafanya biashara wa Marekani kuziona. Wafanyabiashara wa Tanzania waliojitokeza ni less than 30!, kule US tukakuta Wakenya wamejitokeza hundreds!, Waganda zaidi ya 50!.
Tell you what!, 50% ya products walizopeleka Wakenya, zimetoka Tanzania!, wao wamefanya packaging tuu na branding!. Kule US wafanya biashara wengi walivutiwa sana na bidhaa kutoka Tanzania according to samples tulizoonyesha. Zikatolewa big orders, mfano nakumbuka mikeka fulani inatengenezwa kinamama kule Masasi kwa kutumia majani fulani laini, ikatoka order ya 40ft container within the next 6 months!.
Ukisha pew a order, its like an LPO, na inakuwa ni kwako tuu for the period of 6 months, ukishindwa kusupply wewe, after specified period of time, ile order inawekwa online, with details and specifications. Tumerudi, TZ, kind mama wale hawana "the capacity to supply such a big order within a given time!", wakaenda benki kutafuta mikopo, benki wanataka collateral!, kwao supply order ya Agoa, hawaijui!. Wamekwenda TCCA hawakupata msaada wowote!, Board of External Trade kazi kutoa tuu ushauri!. Miezi 6 ikapita bila delivery kufanyika, ile order ya mikeka ikaenda on line!. Yoyote mwenye uwezo wa kusupply hiyo oder kutoka nchi yoyote ya EAC, by then ni Tanzania, Kenya na Uganda tuu!.
Within 2 weeks Wakenya wameisha respond on line kuwa data supply, hivyo ikaondolewa on line that means hate kama wale wamama waliinzaanza, then, deal imeishahama!. Walichofanya Wakenya, walitua Mtwara, wakawasukisha hiyo mikeka vikundi kibao vya kinamama kwa mujibu wa zile needed specifications. Wenzetu wamesaidiwa na serikali yao kuwapatia government guarantee mabenki yao yakatoa fedha!. Within 3 months mikeka ikatua Kenya, wakafanya packaging na branding wao as "products from Kenya!".
Tumekuja kurudi US kufanya followup, huwezi amini, hakuna wafanya biashara wa Tanzania who made it in the first round!, lakini kwenye soko la AGOA, bidhaa zenye origin from Tanzania ila ni "Product from Kenya" zimefurika soko!. Kama ni Mtanzania Mzalendo wa kweli, unaishia kuumia tuu!.
Watanzia ni kama tumelogwa vile!.
Pasco