No, Geza. No. Dont be so naive.
As long as you are identified as the leader of a certain supposedly suppressed ethnic, class or religious group (or worse) if u style yourself as one, it then becomes really difficult to muster countrywide support for the top seat, for the other ethnic, class or religious groups will fear u and wouldnt trust your intentions.
That is Mr. Raila's biggest political blunder that will prevent him from ever ascending to the top seat in the land.
Geza alikuwa sahihi
Ona hali kama hii
Jubilee inarutubisha uchochezi kupitia nyadhifa - Mudavadi
Imepakiwa - Tuesday, June 21 2016 at 11:31
Kwa Mukhtasari
Kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC) Bw Musalia Mudavadi amesema serikali ya Jubilee ndio inakuza kukithiri kwa matamshi ya uchochezi na ukabila nchini kupitia ugawaji wa nyadhifa kuu za serikali kwa misingi ya kikabila.
KINARA wa chama cha Amani National Congress (ANC) Bw Musalia Mudavadi amesema serikali ya Jubilee ndio inakuza kukithiri kwa matamshi ya uchochezi na ukabila nchini kupitia ugawaji wa nyadhifa kuu za serikali kwa misingi ya kikabila.
Kupitia taarifa kwa wanahabari, Bw Mudavadi alisema, "Serikali ya kitaifa imeweka pembeni hitaji la Katiba la kujumuisha kila mkenya. Jubilee imekiuka kipengele nambari 130 kinachoilazimu serikali kuhakikisha inawateua maafisa wakuu wa serikali kutoka matabaka yote nchini hali ambayo imefanya iwe vigumu kupigana na ukabila."
Bw Mudavadi alisema swala hili limepalilia uchochezi nchini na kufanya wachochezi kupata nafasi kubwa nchini kisiasa.
Alisema, "Hakuna hotuba zozote dhidi ya uchochezi zitakazoweza kubadili hali hii ikiwa serikali haitahakikisha kila mtu ahisi kuwa Mkenya."
Aliongeza, “Njia rahisi ya kupigana na ukabila na uchochezi ni kuhakikisha utekelezwaji wa kipengele 130 bila kuzingatia ni nani alipigia nani kura.”
Bila kutaja majina, Bw Mudavadi aliwasihi wakenya kuwakataa na kuwatenga wachochezi huku akisema nia ya wachochezi ni kutumia ukabila kung'aa kisiasa.
Kuzuiliwa kwa siku nne
Matamshi ya Mudavadi yanajiri juma moja tu baada ya wanasiasa wanane kutiwa mbaroni na kushtakiwa mahakamani kwa tuhuma za uchochezi na baadaye kuzuiliwa kwa siku kadha baada ya kunyimwa dhamana.
Wanane hao ni Seneta wa Machakos Johnson Muthama na wabunge Junet Mohamed, Aisha Jumwa, Timothy Bosire, Florence Mutua, Moses Kuria na Ferdinand Waititu.
“Imekuwa hali ya kawaida kwa wanasiasa kuwa mashujaa kwa kuchochea makabila yao dhidi ya watu wengine. Serikali ya Jubilee inazidi kupalilia hali hii na kufanya