Kenyatta afuta baraza la Kibaki

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Rais Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake.

KWA UFUPI
"Kwa mujibu wa Katiba Mpya ya Kenya iliyopitishwa mwkaa 2010, Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mwai Kibaki ilimaliza muda wake usiku wa Aprili 9," alieleza Kenyatta katika taarifa yake iliyosambazwa na Ikulu ya mjini Nairobi.

Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza kumalizika kwa muda wa Serikali ya muungano iliyopita, hivyo kufungua njia ya uteuzi wa Baraza Jipya la Mawaziri litakaloongoza Serikali yake.

Hatua ya Kenyatta inamaanisha kumaliza zama za utawalka wa Rais Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake, baada ya uchaguzi uliofanyika Machi 4 na kumpa ushindi Kenyatta pamoja na mgombea mwenza wake, William Ruto.

Agizo hilo linawahusu wanasiasa waliokuwa katika nafasi za kuteuliwa hasa mawaziri na manaibu wao, ambapo ilieleza kwamba kwa sasa makatibu wakuu wa Wizara ndio watakaoendesha shughuli zote hadi mawaziri wapya watakapotangazwa rasmi.

Taarifa hiyo ilitolewa katika siku ya kwanza ya Kenyatta ofisini akiwa mkuu wa nchi, pamoja na msaidizi wake, Ruto, ambapo walikuwa wakipokea taarifa kutoka kwa wakuu wa usalama, maofisa wa Serikali, mwelekeo wa maandalizi ya bajeti na kupitia kwa mara ya mwisho namna ya muundo wa serikali wanayoihitaji.

Kenyatta afuta baraza la Kibaki - Afrika Mashariki - mwananchi.co.tz
 
Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza kumalizika kwa muda wa Serikali ya muungano iliyopita, hivyo kufungua njia ya uteuzi wa Baraza Jipya la Mawaziri litakaloongoza Serikali yake.
Hatua ya Kenyatta inamaanisha kumaliza zama za utawalka wa Rais Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake, baada ya uchaguzi uliofanyika Machi 4 na kumpa ushindi Kenyatta pamoja na mgombea mwenza wake, William Ruto.
“Kwa mujibu wa Katiba Mpya ya Kenya iliyopitishwa mwkaa 2010, Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mwai Kibaki ilimaliza muda wake usiku wa Aprili 9,” alieleza Kenyatta katika taarifa yake iliyosambazwa na Ikulu ya mjini Nairobi.
Agizo hilo linawahusu wanasiasa waliokuwa katika nafasi za kuteuliwa hasa mawaziri na manaibu wao, ambapo ilieleza kwamba kwa sasa makatibu wakuu wa Wizara ndio watakaoendesha shughuli zote hadi mawaziri wapya watakapotangazwa rasmi.
Taarifa hiyo ilitolewa katika siku ya kwanza ya Kenyatta ofisini akiwa mkuu wa nchi, pamoja na msaidizi wake, Ruto, ambapo walikuwa wakipokea taarifa kutoka kwa wakuu wa usalama, maofisa wa Serikali, mwelekeo wa maandalizi ya bajeti na kupitia kwa mara ya mwisho namna ya muundo wa serikali wanayoihitaji.

CHANZO: MWANANCHI
 
Mpeni nafasi, naamini ataleta mabadiliko.

Hana haja ya kupapatikia biashara na mali, ni tajiri already! mpeni chansi awashangaze wenye mawazo hasi kila siku? hawezi, hawezi, wewe waweza???

Good Luck Uhuru, the road is long, rough and challenging but you will be ...there!
kalieni hawezi hawezi....muone nchi ya wenzenu itakavyoleta mabadiriko, nyie kalieni mazoea, uvivu, ufisadi, majungu na porojo!!!!!!!
:juggle:
 
Itakuwaje kama ICC itawakamata miguu na kuwatia hatiani? Je katiba mpya itawaruhusu waendelee kutawala wakihukumiwa kuwa wahalifu? Hebu wakenya tusaidieni kujibu hili kwamza.
 
Itakuwaje kama ICC itawakamata miguu na kuwatia hatiani? Je katiba mpya itawaruhusu waendelee kutawala wakihukumiwa kuwa wahalifu? Hebu wakenya tusaidieni kujibu hili kwamza.

mimi si mkenya ni mu TZ mwenzio. Lakini ni dhahiri wakenya wameliona na walilijua hili na bado kwa imani yao kwake wamemchagua yeye na Luto. who are we kuanza kutia shaka? let us wish them well.
Hata sisi tuwe tayari ku TAKE RISK na kujaribu uongozi na utawala tofauti.
Mambo ushindani bwana na ndio upimao UBORA.
 
Wa kwetu Tz nimekupata; asante pia kama JF watakuelewa sawa na nilivykuelewa. Kwa Tz 2015 somo la yanayotokea Kenya tusijiwekw mbali nayo kwa sababu Tz ilishiriki kufanya yawe hivi yalivyokuwa; ambayo ni ishara kwamba jaribio limeleta matokeo ambayo ssm watatumia kutimiza agenda yao 2015. Ukisoma yaliyokuja na aktiba mpya ya Kenya sijui kamaTz kwa hali tuliyonayo ita-work. Haya yabakie yetu macho.
 
y do u pipo underate uhuru to me he has brought mote developments than Raila jst compare Gatundu and kibera u wil see a big difference another thing uhuru is the obe that started the economic stimulus plan that has brought about employment to many jst give him time and see
 
Mbona unapiga chenga jibu swali la ICC.
 
ICC na mada ya uzi haviendi pamoja.
baraza la mawaziri walochaguliwa walikuwa katika wizara arobaini. ulimwenguni hakuna taifa linaongozwa na serikali timamu yenye umakini itaruhusu mambo ya aina haya. ni vyema wizara zivunjwe na mfumo na wizara mpya serikalni kujengwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…