mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Rais Kenyatta amewakaribisha watanzania na wengine katika jumuia ya afrika mashariki kwenda Kenya kuchumbia wasichana (kumiliki ardhi) na kuoa huku akijua kuwa wasichana wote wa Kenya walishachumbiwa na kuolewa ( ardhi yote ya Kenya ina wenyewe, na serikali haimiliki ardhi)! Huku akitazamia kuwa na serikali yetu itawaalika wakenya waje kuchumbia Tanzania ambako wasichana wengi zaidi hawajachumbiwa ( ardhi iliyo wazi ni kubwa kuliko iliyogawiwa na serikali ndiyo inamiliki ardhi!)
Hiyo janja ya nyani imeshagonga mwamba! Tutaoleanaje wakati wewe binti zako ulishawaoza wote? Huo ushirika wa kuoleana waufanye na Rwanda na Uganda tuone! Wote hao walishaozesha binti (ardhi) zao!
Hiyo janja ya nyani imeshagonga mwamba! Tutaoleanaje wakati wewe binti zako ulishawaoza wote? Huo ushirika wa kuoleana waufanye na Rwanda na Uganda tuone! Wote hao walishaozesha binti (ardhi) zao!