Kenyatta na maraisi wa Afrika kutokukubali kufikishwa ICC ni double standard

Kenyatta na maraisi wa Afrika kutokukubali kufikishwa ICC ni double standard

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Sipatani sana na wanasiasa kwa sababu moja kuu; wengi wao wamekithiri kwa uongo na ahadi za udanganyifu, kuanzia wenyeviti wa mitaa, wabunge, mawaziri au hata maraisi. Nionyeshe mwanasiasa asiye mdanganyifu nitakuonyesha mtu asiyestahili kuwa mwanasiasa.

Chukulia Kenyatta kwa mfano, raisi wa sasa wa Kenya.

Wakati wa kampeni za uraisi alitoa ahadi kwamba kuwa na kesi ICC si hoja, kwani akifanikiwa kuwa raisi atashirikiana na ICC kikamilifu ili kumaliza suala la tuhuma za ICC dhidi yake - tuhuma nzito kabisa zinazohusu mauaji ya watu wasio na hatia.

Baada ya kuwa raisi Kenyatta ameanza kuimba nyimbo tofauti kabisa; kwanza alianza kampeni ili nchi za Afrika kwa ujumla zijitoe ICC. Hakufanikwa katika hili. Na sasa maraisi wa Afrika katika mkutano wao huko Ethiopia wameamua kuliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiomba/wakidai kwamba mtu anapokuwa madarakani kama raisi asishitakiwe katika ICC!

Natumaini busara ya wale wanaokaa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la sasa ni ya kiwango cha juu kuliko wale walioliandikia ombi/dai la kutaka maraisi waliopo madarakani wasishitakiwe ICC.

Ukitafakari ombi la maraisi wa Afrika, utaona kwamba wanachomaanisha hawa viongozi wa bara langu la Afrika ni kwamba, kukiwa na kiongozi dikteta na muuaji, aruhusiwe kuendelea kuua tu asishitakiwe hadi atakapoacha madaraka ya uraisi.

Pia, hadi sasa nashindwa ni mtu gani mwenye busara kamili anaweza kujitetea kwamba eti ni Waafrika pekee wanaoshitakiwa ICC, sio wazungu. Mtoto wa shule ya msingi? Hivi ni kwa jinsi gani maraisi wa nchi wanaweza kujitetea kwamba mbona wazungu wanaua kama sisi Waafrika lakini hawapelekwi ICC? Khaaa!!! Kwa hiyo, kwa busara zenu enyi waheshimiwa maraisi, mnaona kwamba ili kusawazisha hili kinachohitajika ni kuwaruhusu maraisi wa Kiafrika waue bila kushitakiwa kama wanavyofanyiwa maraisi wa kizungu?

Mtu hadi unachaguliwa kuwa raisi wa nchi yako bado unakosa busara juu ya basic principle kwamba "two wrongs will never make a right?" Just unbelievable.

Kama kweli maraisi wangu wa Afrika wangekuwa na nia na busara ya kutaka kujadili kutoshitakiwa na ICC maraisi waliopo madarakani, wangejadili na maswali yafuatayo;

  • ICC ifanyeje basi, pale raisi dikteta na muuaji yuko katika nchi ambayo katiba yake haina ukomo wa kugombea uraisi (kama Zimbabwe, Uganda nk)? Je, ICC isubiri hadi huyo raisi atakapokufa ndio imfungulie mashitaka?
  • Je, kwa kutaka maraisi waliopo madarakani wasifunguliwe mashitaka ICC, maraisi wa Afrika watakuwa tayari pia kuhakikisha katiba za nchi zote Afrika zina ukomo wa vipindi vya uraisi, viwili visivyozidi miaka mitano kila kimoja?
  • Je, ikiwa maraisi wa Afrika wanataka raisi aliyepo madarakani asifunguliwe mashitaka ICC, watakubali kwamba mtu yeyote mwenye tuhuma za mauaji asiruhusiwe kugombea uraisi katika nchi yeyote, eidha kabla hajawa raisi au kutogombea muhula mwingine ikiwa yeye ni raisi tayari? (kwa mantiki hii Kenyatta asingegombea uraisi Kenya kwa kuwa alikuwa na tuhuma tayari, au asiruhusiwe kugombea uraisi awamu ya pili)

Haya ndio mambo ya msingi ambayo kama kweli maraisi wetu wangepaswa kuyajadili. La sivyo wanaongea vitu ambavyo vinapoteza muda si wetu tu bali hata wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na binafsi nawasikitikia hao waliowachagua kuwa maraisi. Wanatutia aibu sisi Waafrika wengine kudai mambo yanayolinda usalama wa wana Afrika yaondolewe kwa sababu za ki Abunuwasi kama wanazozitoa.
 
Kwamba sitting president asifikishwe ICC haitakiwi kuwa kikwazo kwa mahakama hiyo.Katiba za nchi zimtake Rais huyo ajiuzulu kwanza ndio afukishwe kwa korti.Mtuhumiwa wa mauaji dhidi ya wananchi wake kwa kweli hastahili kuendellea kuwaongoza wananchi hahao kabla ya ukweli kubainika.
Wanadhani UN ni genge la wauaji kama

wao.
 
Kinachonisikitisha ni press conference zetu. Waziri wa mambo ya nje anawatapikia waandishi hata kumuuliza tu: 'kujiondoa ICC ni kwa maslahi ya nani kipindi hiki ambapo AU haiwezi kumkoromea dikteta yeyote aliepo na ajae?' Wamejadiliana nini kuhusu ugaidi unaowagusa wananchi wengi kuliko ICC inayowahusu viongozi wawili?
Waandishi acheni kua maripota tu.
Kwa hali hii wazungu wataendelea kututukana sana.

tragedy of the commons
 
Tunahitaji viongozi makini ktk bara letu. kwa maana nyingine marais wote wa africa wana udictator na ndio maana wanapitisha maamuzi ya kipuzi kama haya. Mungu tusaidie
 
Africa bara langu!!itakuwa kuna laana sio bure...na tz kujitoa inawezekana si unajua wazee wa ndiooo walivyo wengi.
 
Kifungu kimeafikiwa?... NDIYOOOO.... Katibu,shughuri inayofuata....
 
I support Synthesizer. ICC was passed by the AU and it appears they passed it to discipline their citizens only whereas on the contrary it was more applicable to discipline presidents who in their country are practically above the law. The presidents should not decide matters affecting them when they break a law. To me the ICC is more to presidents with acts against humanity and in general the laws of their country. Presidents need to consult their people in a referendum.
 
Tunahitaji viongozi makini ktk bara letu. kwa maana nyingine marais wote wa africa wana udictator na ndio maana wanapitisha maamuzi ya kipuzi kama haya. Mungu tusaidie

Mkuu Mungu atasaidia sana, ICC na International Community imesha wajulia waharifu walivyo, wanapenda sana kutumia Mob-psychology kujinasua kwenye majanga walitengeneza wenyewe na wakati mwingine wanatumia mbinu za ku-falsify matokeo ya kura ili wateuliwe Urais na Umakamu wakiwa na imani kwamba hilo tu ndio itakuwa kinga ya wao kutofikishwa mahakani na hicho ndicho wanasimamia mpaka sasa; visingizio chungu mzima eti "Wazungu wanataka kudhalilisha Wafrica" kwani Waserbia waliofikishwa the Hague ni Wafrica?

Binafsi naona aibu sana nikiskiliza hoja za Viongozi wetu Wa Africa nzima wakijenga hoja dhaifu kabisa, kwa nini wanataka ku-support Viongozi wanao tuhumiwa kwa mauaji ya haraki? Je na wao wana traits kama za wenzao au? Koffi Anani na Viongozi wengine waliwahi kutoa tahadhali, lakini si unajua tena Wafrica tuliyvo wali wapuuzia! Kibao kinawagehukia wana anza kulahumu wazungu wote wakati Prosecutor ni Mwafrica mwenzetu - binafsi I salute HER, yuko serious na waswahili kwa kuwa anatujuwa tulivyo, tatizo letu ni ulevi wa madaraka ndio tushio la Africa - sisi ni watu hatari sana hatutaki kabisa demokrasia ya kweli, akili zetu kuendesha nchi zetu kimafia mafia, nepotism, tribalism and all isms you can imagine.

Tuwe wakweli hapa, bila ya ICC Wafrica hatuwezi kupona dhidi ya watawala dhalimu wanao endesha nchi zao ki-imla? Wafrica tumejaa visingizio chungu mzima na mechezo ya kuhigiza tu: Watufafanulie ni wapi ICC iliwahi kusema kwamba nchi takribani 52 na ushee za Kiafrica zinapashwa kuburuzwa mahakamani, watuhumiwa wawili tu ndio wasimamishe Africa nzima isifanye kazi - kitu gani wanaogopa kama hawana hatia, kwa nini hawataki kusimama kiume wakajitetea; badala yake wanaishia kwenye njama za ku-mobilize Africa nzima ili iwatetee/kingias kifua - kuna kitu wana hofia si bure.
 
Nakubaliana na Sysnthesizer asilimia 100. Rais Uhuru anatakiwa awaombe radhi wakenya kwa kuwa aliwadanganya. Ni kweli kabisa kwamba alipokuwa kwenye campaign alisema suala la ICC ni lake binafsi na kwamba atashirikiana na mahakama hiyo ili asafishe jina lake. Sasa iweje anaanza ngonjera na sarakasi baada ya kuwa Rais? Kinachoonekana ni kwamba hakuwa anatafuta urais ili awatumike wakenya bali urais iwe kama daraja la kutokea. Pia naamini kwamba wakati wanatafuta kuongoza nchi Uhuru na Ruto walifahamu fika kuhusu kifungu nr 27 cha Rome Statue ambacho kinasema kwamba wadhifa wa mtuhumiwa (awe mkuu wa nchi, mbunge, n.k) hautatoa kinga ya au kutoshtakiwa au kupunguziwa adhabu. Pia kifungu cha 63 kinachomtaka mstakiwa awe mahakamani muda wote wa kesi. Sasa iweje waanze kupig kelele kana kwamba hawakuwa wanafahamu mambo haya? Kwa kweli inabidi wawaombe wakenya radhi, vinginevyo washirikiane na ICC ili wasafishe majina yao.
 
cart1610-595x423.jpg
 
Back
Top Bottom