JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Rais wa Kenya amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kile ambacho anadai kilipangwa kufanya na Makamu wake wa Rai, William Ruto, kusimamia mipango ya kumfanyia hujuma na kushitaki.
Kenyatta, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Kikuyu ambao walimtembelea Ikulu Jijini Nairobi.
Amesema Ruto alikuwa na uchu wa madaraka makubwa na alitaka kufanya hivyo kwanza kwa kuchochea upinzani ndani ya Chama cha Jubilee ili amzidi kete bosi wake.
Kenyatta ameeleza kuwa hata ule mpango wake wa Machi 2018, kukutana na kupeana mkono na mpinzani wake mkuu (Odinga) ilikuwa maalum ili kuzuia Ruto kuhujumu utawala wake na kuingia mamlakani kupitia mlango wa nyuma.
Kenyatta amemshutumu Ruto kwa kupinga maridhiano na Odinga ambapo alikuwa akitaka aendelee kuonyesha misimamo mikali dhidi ya kiongozi huyo wa ODM.
Wakati zikiwa zimesalia siku 135 kabla ya uchaguzi wa Rais, tayari Rais Kenyatta ameonyesha msimamo wake wa kumuunga mkono Odinga na kuwashawishi wananchi na vyama mbalimbal kumuunga mkono kuliko Makamu wake huyo.
Source: Citizen Digital