Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Nimejaribu kufuatilia sana purukushani za uchaguzi wa Kenya mpaka sasa. Nimesoma haya:
1. Katiba ya Kenya ni zuri sana na haijatoa mwanya wa mtu kujiinua;
2. Kenyatta anaroho ya kutokubali demokrasia ila anafungwa na Katiba. Natolea mfano wa matamushi aliyotoa juu ya wale walioamua kesi ya uchaguzi. Amewaita kwa maneno mengi sana. Ila kubwa ni lile alilosema ni "wakora". Sina maana kamili kwa kiswahili cha kwetu, ila naamini anamaanisha wanyang'anyi. Ameendelea kusema kuwa majaji wote waliompigia kura za kuopinga uchanguzi wamefanya maamuzi hayo kisiasa. Hili ni kweli? Ni jambo la kujiuliza.
Kwa sababu hiyo, leo Chama cha Mawakili nchini Kenya (LSK) kimemkosoa Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake.
Rais wa LSK Isaac Okero alimkosoa Rais Kenyatta kwa kumtaja Jaji Mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa wamekosea.
Okero amesema Matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya.
Wewe unasemaje hapo? Kenyatta ni mwanademokrasia au ni Katiba imemfunga?