Mzee Kimamingo
JF-Expert Member
- Mar 31, 2024
- 1,861
- 4,462
Kama Kichwa kinavosema.
Baada ya kumaliza Chuo 2018 na kufanya kazi kwenye Sekta binafsi niliona ni kupoteza muda na mateso pale unapokaa miezi hadi mitatu bila mshahara nikaamua niache kazi na kujiajiri kwa kufanya biashara.
Ila sijawahi kupigika na maisha kama 2022 mwaka nilioamua kufanya biashara kwa kuwa Manispaa kila siku wanatimba Dukani kutaka ukate leseni hujakaa vizuri TRA hao apo bado Kodi ya fremu kibaya zaidi Ni Chuma ulete asee Tegeta kwa ndevu mlininyoosha.
Ndio nilipoamua kuzama Ajira portal na nikapiga interview moja na kupata ila ndio nikarushwa Halmashauri moja kongwe huku Mikoa ya Kusini.
Kero za huku sasa mpaka sasa.
1. Pesa ya kujikimu mwezi wa 6 huu sijaipata yote imelipwa nusu tu.
2. Miezi 6 sijawahi pata Kasafari kokote wala posho yoyote.
3. Ofisi ya uhasibu ni MIUNGU watu wao ni kawaida kula haki yako wakisingizia hawana kifungu.
4. Wewe upo tu unalinda ofisi wenzako wanaenda kufanya kazi za posho bila kukwambia.
5. uchawi na kulogana pia kupo baada ya kukuta nazi imevunjwa asubuhi mlangoni kwa ofisi yetu .
Mliopo muda mrefu huku kwenye Halmashauri hali ipoje??