Kero ndogo ndogo ndani ya tasnia ya muziki wa kizazi kipya (bongo flavour).

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,095
Reaction score
22,731
1.Muziki wa kisasa umegawanyika katika makundi haya (a)Nyimbo za taratibu kama SOUL,R&B,urban JAZZ,na Zouk,country(b)Nyimbo zenye kubeba hisia za kimapinduzi au changamoto kama HIP HOP,REGGAE,(c)Nyimbo za kuchezeka au kubanjuka kama vile Pop,rumba,charanga, na ROCK, na Blues( ndio blues ni mziki wa kasi tofauti na wengi wetu tunavyozania kuwa ni mziki wa taratibu sana kama za akina celine dion na akina whitney huston)

Sasa,unakuta mfano msanii wa bongoflavour anajitambulisha kuwa yeye ni msanii wa R&B,sikiliza sasa utumbo anaoimba na kuuita R&B utacheka.Unakuta mtu anaimba mduara,kesho reggae kesho huyo huyo ana utamkuta na babu yusufu wanaimba taarabu.Hii sasa siiti kuwapa mashabiki zako ladha tofauti...ila ni kuwachanganya kuhusu wewe unawakilisha nini hasa kwenye tasnia soon wanakupotezea unaanza kusema umelogwa kumbe mwanga ni wewe mwenyewe.

2.Kupotea muda mrefu bila kujulikana kuwa umeacha muziki au unasubiria tukuulizie sana ndio uje tena hewani.

3.Wasanii kupenda umaarufu wakati mchango wao kivitendo ni 0% katika tasnia.Kazi tu kujiweka weka mbele ya vyombo vya habari ili utajwe uonekane maarufu kumbe hauna lolote.

4.Wasanii wanaovuma wakishaanza kufulia kuanza kujiita magwiji,legendary,au wakongwe....wakati tukikuangalia kwenye tasnia hata miaka 20 hauna......wakongwe huitwa wasanii ambao wako kwenye tasnia mia 40 na yeye ukimtizama anakuwa ni mzee kweli kweli mfano ni ngurumo.

5.Vijana waliokosa kazi au muelekeo wa maisha kuvamia fani ya mziki wakati hawana kipya cha kuchangia....cha zaidi hapo atataka awe richy mavoko,diamond, au alikiba wa pili badala ya kuwa na upekee wake.Kazi kubwa wanachofanya hapa ni kuzipatia studio pesa za bure kwa kutengenezewa muziki unaofanana.Mwisho wa siku unaharibu hadi heshima yako mtaani kwa kujichoresha kufanya vitu usivyo na uwezo nao.




Wadau changieni kwa kuongezea kero nyingine mnazozifahamu ili wadau wazione wajirekebishe.
 
Mimi nakuunga mkono hapo kwenye namba 5,yaani sasa hivi imekua kero kila mtu anataka kuwa msanii,wanachokiimba hakionekani nakasirika sana
Umefika wakati wa vijana kuwa na fikra tofauti za kutoka kimaisha sio kutegemea mziki pekee
 
ndugu yangu kuanzia no 2 hadi 5 uko sahihi. but hapo no1 napingana na wewe kidogo mkuu....kwa mtazamo wangu music ni biashara so huwezi kumteka mzee with hip hop so its not bad for artists to try different kind of music just to target business hata hao kina whitney walimix some songs for the same purpose marketing
1.I wanna dance with somebody....whitney this is not slow its dancing music its like pop and she was an rnb artist
2.I drove all night....celine dion this is pop and she is rnb artist..
3.ukija nyumbani ..mambo ya pwani hii ngoma solo thang aliitowa katika hip hop na mduara na ilifanya vizuri
4.jay dee we know her as rnb artist but she does mixing different flavor and she is doing good
5.j nature siku hizo tulimjua kama hip hop artist next thing akatoa ile ...kwani wao wameweza wana nini na sisi tushindwe tuna nini...haikuwa hip hop lakini ilifanya vizuri
kujaribu aina nyingine ya muziki huo ndio USANII msanii anatakiwa awe mbunifu...jaribu jazz soul rnb blues so ukipafom kwa wazee unawaua na jazz wamama soul vijana warushe mipop na rnb ukienda mkuranga unawachapa na mduara
huu mtazamo wangu tuu
 
motsepe; Umetisha mkali ......but kwa udadisi nilioufanya imeonekana wasanii wanaodumu na staili moja wanajenga jina imara na rekodi kali zaidi ya wasanii wanaobadili style kila kukuchapo.
 
Last edited by a moderator:
Mziki ni biashara, kama style haimake ela basi hai make sense badili kwenda style inayo make ela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…