KERO: Tegeta Kwa Ndevu Machinjioni uchafu umekithiri

KERO: Tegeta Kwa Ndevu Machinjioni uchafu umekithiri

Willima

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
26
Reaction score
39
Kero hii ni kubwa na inasumbua watu wengi sana, na uchafu huo unatokana na kuwa karibu na jalala na pia kuwa karibu na machinjio ya ng'ombe.

Uchafu huu unasababisha harufu mbaya inayo fika hadi kwenye nyumba za watu, na pia kuanikwa kwa mbolea ya ng'ombe kunasababisha uwepo wa wadudu kama nzi na mbu ambao pia ni hatari kwa afya ya binadamu, pia kunikwa kwa mbolea hiyo kunasababisha uchafu hasa kipindi cha mvua kwasababu kunakua na tope la mbolea hiyo iliyo anikwa.

Pia uwepo wa mto ambao pia uko karibu na makazi ya watu na pia uko karibu na jalala na uchafu wa jalalani kuangukia mtoni na kusababisa mazingira machafu zaidi.

Pia miundombinu ni mibovu, kuna mfumo mbovu wa maji taka na barabara mbovu.Tunaomba serikali iboreshe miundombinu na kusimamia suala la usafi katika eneo hili
 
Mbunge yupo busy na visa za kuwapelekeni USA, msikimbilie humu wakati mmeshindwa kutumia nguvu ya kura uliyopewa, ni kuandaa passport tayari kuruka kwenda Miami Beach ⛱
 
Back
Top Bottom