Tunachokitaka wananchi ni barabara irekebishwe kwa kiwango cha lami , zege au morum. Kuanzia pale nile perch mpaka kakebe.
Haiwezekani gari za kakebe ziishie mhandu kanisani kisa barabara mbovu na mamlaka ipo. Kuna kidaraja uchwara kilijengwa maeneo ya kakebe shule ya msingi mpaka leo kameachwa vile vile.
Nimeona leo wafanyabihashara wameambiwa wafanye usafi barabarani ila haiondoi ukweli kua barabara inakua na matope makali na madimbwi ya maji mvua ikinyesha.
Tunataka barabara ya kiwango ili magari yapite kwa uhuru,.. Watu wapite kwa uhuru. Mandari ya machinjioni kakebe yapendeze na uchumi uzidi kukua zaidi sio blaa blaa.