Wadau habari za mchana
Kuna hili jambo la kulipishwa gharama ya malipo ya Serikali namawakala nilikuwa nalisikia kwa watu leo limenikuta. Nimeenda kufanya malipo ya TZS 560,000/= kwa CONTROL NUMBER 991440462684, Wakala wa Benki ya CRDB kaniambia nilipe TZS 1500/=. Nilipouliza ni malipo ya nini, akanijibu gharama ya huduma kwa mteja hawalipwi kamisheni kwa malipo ya serikali. Wajuzi wa mambo naomba kujua hizi gharama ni haki au tunapigwa??