Kero ya maji inanisukuma nikaichanechane bendera ya CCM iliyopo hapa ofisini ili labda nisikike kirahisi

Kero ya maji inanisukuma nikaichanechane bendera ya CCM iliyopo hapa ofisini ili labda nisikike kirahisi

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Sio siri huku tunako ishi mitaa ya Goba maji yamekuwa bidhaa adimu kiasi kwamba unalazimika kusubiria maji utadhani maji ya msaada.

Hali hii inanikera sana huwa najiuliza hivi kazi ya chama tawala ni ipi!? Ni kutuimbia tu manyimbo? Kama ni kuisimamia serikali mbona serikali haileti maji akati kodi inakusanya!?

Juzi kati hapo tumepigwa changa la macho na ziara za awesu maji yakatoka siku alizokuwa hapa alipoondoka tu na maji yameondoka.

Najua kisheria ni kosa lakini hali ikiendelea hivi mimi nitaenda kuichana bendera ya ccm ili nifikishe ujumbe kwa njia rahisi kuwa wananchi tumechoka kupuuzwa.
 
Kachane hiyo bendera ungojee mchango wa mil 5 kutoka X.
 
Jimbo la kibamba lote miundombinu ni ya hovyo sana ukiondoa tu Huku barabara morogoro. Maji hakuna, barabara hakuna, hospitali hakuna hata chuo Cha afya hakuna, umeme unazimikazimika. Halafu Mbunge wa huko Abbas Mtemvu akiwa anachangia bungeni ni kumsifia Rais Kwa kazi nzuri. Hata waziri wa maji Huwa anawapiga siasa tu .

Ni Bora Hilo Jimbo likajitenga na kuwa Nchi inayojitegemea ili watumie vyema rasilimali za huko na siyo kukamuliwa tozo Kila siku na kutumiwa na Samia kwenye msafara wake wa magari 400.upuuzi kabisa.
 
Kachane hiyo bendera ungojee mchango wa mil 5 kutoka X.
Uoga haujawahi kuleta suluhu ya matatizo ya watu hatuwezi kuishi kwa kuogopa kwenda jela huku baadhi ya watu wakineemeka kwa kodi zetu kamwe
 
Back
Top Bottom