Kero ya mitandao ya simu kushikilia pesa za wateja pindi miamala inapofeli

Kero ya mitandao ya simu kushikilia pesa za wateja pindi miamala inapofeli

Sensei Tai

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
168
Reaction score
466
Kuna hii tabia ya mitandao ya simu kushikilia pesa za wateja pindi miamala inapofeli huwa inakera sana

Ijumaa iliyopita nilifanya muamala toka akaunti yangu ya Tigopesa lakini cha ajabu pesa ilikatwa lakini kule nilipokua nadeposit muamala mpaka sasa hauja reflect na pesa haijarudishwa kwenye akaunti yangu ya Tigopesa.

You can imagine since last Friday mpaka leo wameshikilia pesa yangu wakati siku ileile niliwapigia simu wakanambia within 24 hours pesa yako itarudishwa kwenye account yako au utaiona kule ulikokua unadeposit.

Hivi haya makampuni yapo serious kweli ? Unakaa na pesa ya mtu kwa zaidi siku tano na ume relax kabisa ofisini

Kwanini wasirekebishe system zao ili once muamala unapofeli ndani ya dakika 5 mpaka 10 pesa irudi kwenye akaunti ya mteja, halafu kibaya zaidi kila unapopiga customer care yani utadhani ndo unawaambia tatizo lako kwa mara ya kwanza kumbe umeshapiga simu hadi umechoka

Hii mitandao ya simu inahitaji maboresho makubwa
 
Back
Top Bottom