A
Anonymous
Guest
Eneo la Iyumbu NHC Dodoma limekuwa na tatizo sugu la maji kwa zaidi ya mwaka sasa, mwanzo sababu mbalimbali zilikuwa zikitolewa ikiwamo kutumia kisima kimoja cha maji na chuo cha UDOM hivyo kutokidhi mahitaji, lakini pia udogo na wakati mwingine kuharibika kwa pampu za kusukuma maji hivyo kaya nyingi ziliamua kufunga matank ili angalau kuhifadhi maji ambayo hapo awali yalikuwa yakitoka walau siku mbili kwa wiki japo kwa masaa machache, miezi 6 sasa tatizo limezidi kuwa kubwa zaidi maji yanaweza kutoka na mara moja kwa wiki ama hata kwa wiki mbili na presha yake ni ndogo hayafiki kwenye tanki na hakuna taarifa yoyote inayotolewa kwa wananchi
Kipindi cha hivi karibuni nimegundua kuwa mtu anayehusika kufungua maji analipwa na baadhi ya watu kiasi cha pesa ili kuweza kuwafungulia maji kwa presha kubwa ili kuwajazia matanki yao huku wengine wakiendelea kukosa hii huduma ya maji.
Kinachoshangaza zaidi bili za maji za duwasa zinatoka kama kawaida hazitofautiani sana na kipindi upatikanaji wa maji ulivyokuwa afadhali na sasa ambapo naweza kusema huduma ya maji hakuna kabisa. Bili hizi zinapotoka ukichelewa kulipa hata kwa muda mfupi wanakuja kukata maji haraka sana na utarudishiwa tena utakapo lipa na faini kubwa juu yake.
Mweji january Waziri wa maji alitembelea eneo la udom pamoja na Iyumbu na kuahidi kuboresha upatikanaji wa maji eneo hili lakin mpaka sasa huduma hii imezidi kuwa mbovu zaidi kuliko hata kabla ya kuja kwake.
Ninauliza mamlaka ya maji inatambua shida ya maji iliyopo Iyumbu NHC dodoma na wamechukua hatua gani.
Pia
Kuna watu wanafanya biashara ya kusambaza maji kwenye eneo hili ambao pia nahisi wanahujumu miundo mbinu ya maji katika eneo hili ili waweze kuendeleza biashara yao ya maji.
Ninaomba mamlaka husika zifanye uchunguzi na kutatua kero hii sugu ambayo imefanya pia kuwe na mianya ya rushwa kwa watendaji wa DUWASA.