oko majimaji
JF-Expert Member
- Nov 11, 2016
- 790
- 2,079
Habari Mabibi na Mabwana.
Naomba nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye kero, Kero hii inihusiana na usafiri wa umma kwa wakazi wa Buza ( kwa Lulenge hadi Kanisani). Hapo awali usafiri wa daladala kutokea maeneo tofauti kwenda Buza gari zilikuwa zinaenda hadi Buza Kanisani ( mwisho wa gari) lakini kuanzia jana tarehe 03 June 2024 daladala zote zimesitishwa kufika Buza Kanisani na zinatikiwa ziishie na kugeuzia Buza kwa Mama Kibonge.
Hili ni tatizo kwa wakazi wa maeneo ya kwa Lulenge hadi Kanisani kwa sababu ukitaka kwenda Kariakoo, Makumbusho, Mnazi Mmoja na kadharika itakubidi ukodi bodaboda au bajaji ili ufike stendi kwa Mama Kibonge ndio upate usafiri wa kwenda hayo maeneo niliyotaja.
Kutokana na kipato kidogo cha wakazi wa maeneo hayo ya Buza kwa Lulenge hadi Kanisani wamejikuta wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya usafiri, tatizo hili litakwenda kuwaathiri moja kwa moja wadogo zetu wanafunzi wa sekondari wanaosoma maeneo tofauti zaidi hawa wakike maana kwa vipato vyetu huku ni ngumu mzazi kumpa nauli ya pikipiki kila siku.
Pia kinachotusikiisha zaidi Buza Kanisani kuna kituo cha kugeuzia daladala kilijengwa na hakijatumiwa, kwanini wasiruhusu daladala zifike hadi Buza kanisani ndio zirudi zipitie hapo kituoni kwa Mama Kibonge kuliko kuwachosha watu watembee zaidi ya kilomita mbili kufata usafiri wa daladala.
Kupitia andiko hili nina imani mkuu wa mkoa Albert Chalamila litamfikia na ataona namna gani ya kutatua kero hii kwa maslahi mapana ya wananchi wa Buza.
Ahsanteni na niwatakie kazi njema.